emedichi
Member
- Mar 1, 2008
- 46
- 6
Wakati barabara tanzania ni mbovu, usafiri wa anga unakua hatari zaidi. Sa hivi labda punda tu ndio salama. Why? Why? Why?
Ndege yaanguka Arusha
2008-07-05 09:37:08
Na Cynthia Mwilolezi, PST Arusha
Abiria wote akiwemo rubani waliokuwa wakisafiri kwa ndege ndogo ya Idara ya Wanyamapori mali ya serikali, wamekufa baada ya ndege hiyo kuanguka eneo la Monduli, mkoani Arusha.
Ndege hiyo ilianguka baada ya kupoteza mawasiliano muda mfupi iliporuka katika kiwanja kidogo cha Kisongo, nje kidogo ya mji wa Arusha.
Tukio hilo limekuja takriban mwezi mmoja tangu helikopta mali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ianguke na kuua watu sita mkoani Arusha.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Bw. Basilio Matei, aliwataja marehemu wa ajali hiyo kuwa ni pamoja na rubani wake, Kapteni Pius Ngwalali na abiria wawili, Mariam Zakaria ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Wanyamapori jijini Dar es Salaam na afisa mwingine idara hiyo, Stephen Mahinya.
Kamanda Matei alisema kuwa wakati ndege hiyo iliyotoka Dar es Salaam na kutua katika kiwanja cha Kisongo kwa lengo la kujaza mafuta ikiruka kuelekea Loliondo, walikuwepo watu waliokuwa wakiwasubiri.
Hata hivyo, alisema baada ya kuona muda unazidi kupita, walitoa taarifa polisi na hivyo kazi ya kuitafuta ikaanza.
Kamanda Matei aliongeza kuwa, ndege hiyo yenye namba za usajili 5H aina ya C 182, iliondoka jijini Dar es Salaam juzi.
Alisema baada ya kujaza mafuta, iliruka saa 6:00 mchana kuelekea Loliondo, wilayani Ngorongoro kwa ajili ya masuala ya kazi za wanyamapori lakini ghafla ilikata mawasiliano.
Hata hivyo, ndege hiyo ilipatikana jana mchana katika milima ya Monduli huku rubani na abiria wake wakiwa wamekufa.
Baadhi ya watu walioiona ndege hiyo walisema haikuungua moto mahali ilipoangukia kama ilivyokuwa ikihofiwa.
Kamanda Matei alisema uchunguzi wa chanzo halisi cha ajali hiyo unaendelea.