AJALI: Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole wapata ajali mkoani Kigoma

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
0fc53073dedbb1d39f447357cbbfcbb8.jpg


Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole umepata ajali katika eneo la Kijiji cha Nyamidato, Kata ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Vx yenye namba za usajili T150 CWE iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Kibuta wakati wakielekea katika ziara ya kiongozi huyo wilayani Kakonko, mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kulia.

Kwa mujibu wa Kamanda Otieno, waliojeruhiwa ni pamoja na Katibu wa CCM mkoa Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa UVCCM Sylivia Sigura pamoja na Katibu Mwenezi, Feruz ambao wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo kwa matibabu.

Polepole amewasili leo mkoani Kigoma na kupokelewa wilayani Uvinza akitokea mkoani Tabora ambapo atakuwa Kigoma kwa takribani siku tatu.

Chanzo: Azam Tv
 
Ajali zikiwa za kwao ni kupasuka kwa tairi. Refer tena ya RPC Arusha.
Zikiwa za wengine ni mwendo kasi wa sereva.

Polisi wetu wa siku hizi bwana!!

Mungu anawaona. Hamhitaji pole maana mmezuwia wengine wasifanye mikutano ila nyie mnazunguka nchi nzima.

Tutawakabidhi kwa Mungu kwa njia ya maombi nae atatujibu...
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom