Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,601
- 6,014
Basi linadaiwa kusababisha ajali jana mkoani Morogoro lilibeba mashada ya maua, dereva aliposimamishwa kwa mwendo kasi alidai Wanawahi Msibani
Taarifa za kuaminika kutoka kwa abiria ni kuwa gari hilo halikubeba maiti na abiria wote waligeuka waombolezaji kila gari liliposimamishwa.
Na taarifa za hivi punde kutoka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilim amesema idadi ya waliofariki dunia imeongezeka kutoka 7 mpaka kufikia 9.
My Take:
Gari ikisafirisha maiti huwa inapewa vibali na kuna nyaraka za kusafiri nazo,JE ZILIHAKIKIWA?, Lakini je Gari yenye maiti inaruhusiwa kukimbia zaidi ya mwendo halali?
Jeshi la polisi msikwepe hili lawama.
====
Watu Tisa wamefariki dunia huku wengine 23 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Oil Com Manispaa ya Morogoro.
Ajali hiyo imehusisha magari matatu gari la Abiria Toyota Coster yenye namba za usajiri T686 DUK, iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya, Gari ndogo aina ya Crester yanye namba za usajili T563 ASA pamoja na Lori la Mizigo kampuni ya Dangote.