Ajali Mlimani City: Yadaiwa watu watatu wamefariki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,965
Habari Wakuu,

Nimepata taarifa ya ajali maeneo ya Mlimani City ambayo imetokana na lori kuacha njia na kuwazoa wafanyabiashara wanaouza bidhaa mbalimbali nje ya Mall ya Mlimani City.

Taarifa zinaeleza kuwa watu 3 wamefariki pale pale.

Naendelea kufuatilia na nitawajuza hapa.

Jaman kuna ajali hapa Mliman City lorry la Mafuta limewabana watu kweny mtaro ina sikitisha sana. Daaaah Mungu awaepusha na kifo. Watu kama kawaida wamejana, wanataka kuiba mafuta. Polisi wanafanya kazi ya ziada kuwafukuza hawatoki.
1574548412466.png

======

UPDATES:

Watu watatu wamefariki, mmoja amejeruhiwa kufuatia ajali ya lori la mafuta mali ya Kampuni ya Transfuel Logistics Ltd Iringa (T828 DCB) lililokuwa likitokea Ubungo kuelekea Mwenge kupoteza mwelekeo & kugonga Kituo cha Daladala Mlimani City, leo Nov 23. Miili imechukuliwa na polisi
 
Jaman kuna ajali hapa Mliman City lorry la Mafuta limewabana watu kweny mtaro ina sikitisha sana. Daaaah Mungu awaepusha na kifo. Watu kama kawaida wamejana, wanataka kuiba mafuta. Polisi wanafanya kazi ya ziada kuwafukuza hawatoki.
 
Waendesha malory wengi wako mwendo kasi sana. hapo mliman city kuna taa mbili za barabara bado mbele kuna njia ya mzunguko ila magari yanavyo pitaga hutaamini ni sehem ambayo kuna njia za wapita kwa miguu(zebra)
 
Barabara zote zimefanywa masoko ! Mungu anatusitiri sana ! Na roho zao zipumzike kwa amani !! Mamlaka husika siku hizi zinafanya nini !?
Hivi kwanini tunaruhusu watu wafanye biashara hata kwenye maeneo ambayo ni wazi hakutakiwi liwe na biashara yoyote?
 
Poleni mliofikwa na hayo, na pia ni muhimu tena swala la biashara za barabarani kuwa reviewed, wachuuzi wadogo wadogo waone haya madhara liwe somo, mamlaka ziangalie namna sahihi ya kufanya waingize vipato vyao katika hali salama.
Ndugu Stroke, tatizo tunafanya siasa katika kila jambo na hii ndio sababu mambo yanakuwa hovyo hovyo.

Leo serikali ikisema isafishe barabara na wauzaji wawe na maeneo rasmi ya kufanya biashara,upinzani watatumia huo mgogoro kama mtaji. Ndivyo hivyo pia serikali inawatumia kama mtaji.

Binafsi siungi mkono kabisa huu utaratibu wa kila sehemu mjini kuwa soko.
 
Poleni sana wafiwa na majeruhi get well soon,kwakuwa kuna lori la mafuta polisi fanyeni kazi ili kuepeusha madhara ambayo yanaweza kutokea.
 
Ndugu Stroke, tatizo tunafanya siasa katika kila jambo na hii ndio sababu mambo yanakuwa hovyo hovyo.

Leo serikali ikisema isafishe barabara na wauzaji wawe na maeneo rasmi ya kufanya biashara,upinzani watatumia huo mgogoro kama mtaji. Ndivyo hivyo pia serikali inawatumia kama mtaji.

Binafsi siungi mkono kabisa huu utaratibu wa kila sehemu mjini kuwa soko.

ili swala ni changamoto kubwa. lakini madhara yake ndio kama haya.
 
Poleni mliofikwa na hayo, na pia ni muhimu tena swala la biashara za barabarani kuwa reviewed, wachuuzi wadogo wadogo waone haya madhara liwe somo, mamlaka ziangalie namna sahihi ya kufanya waingize vipato vyao katika hali salama.
Wafanyabiashara ndogo ndogo wamevamia sana barabara na ni hatari sana kwa maisha yao,mbona wakifanya sehemu za sokoni zilizotengwa watu wataenda tu bila wasiwasi? Siasa nyingine ni upuuzi.
 
Back
Top Bottom