Ajali Mlimani City: Yadaiwa watu watatu wamefariki

Habari Wakuu,

Nimepata taarifa ya ajali maeneo ya Mlimani City ambayo imetokana na lori kuacha njia na kuwazoa wafanyabiashara wanaouza bidhaa mbalimbali nje ya Mall ya Mlimani City.

Taarifa zinaeleza kuwa watu 3 wamefariki pale pale.

Naendelea kufuatilia na nitawajuza hapa.




======


UPDATES:

Watu watatu wamefariki, mmoja amejeruhiwa kufuatia ajali ya lori la mafuta mali ya Kampuni ya Transfuel Logistics Ltd Iringa (T828 DCB) lililokuwa likitokea Ubungo kuelekea Mwenge kupoteza mwelekeo & kugonga Kituo cha Daladala Mlimani City, leo Nov 23. Miili imechukuliwa na polisi
Polisi wawaachie wachote mafuta ili lori lipungue uzito na wachomoe betri ili mafuta yaliyobaki yakauke.
 
Image may contain: outdoor


Leo barabara ya Sam Nujoma, karibu na Mlimani City. Imethibitishwa mtu mmoja amekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Serikali iamke sasa na kutahadharisha machinga kuwa upangaji wa bidhaa pembeni kabisa mwa barabara unaofanywa ni hatari.

Sio siri machinga ni mtambo wa kura lakini wataendelea kuteketea kutokana na ajali kama hizi zinazotokea kila siku nchini.
 
Tatizo ni wanasiasa, siku za nyuma Serikali iliwazuia wamachanga kufanya biashara sehemu zisizo ruhusiwa wapinzani wakaja juu kuwatetea na kuwatumia kwenye kila maandamano ya kupinga Serikali huku wakiaminishwa kuwa wanaonewa. Serikali baada ya kuona wapinzani wanawatumia wamachinga kisiasa pale wanapozuiwa na Serikali kufanya biashara sehemu zisizo ruhusiwa, Serikali ikaamua kuwaruhusu wafanye biashara kwa uhuru na ndipo wapinzani wakakosa watu wa kuwaunga mkono wanapoitisha maandamano. Tatizo la siasa za nchi hii ni za kubomoa siyo kujenga ndiyo maana serkali ikifanya vibaya wapinzani wanashangilia na ikifanya vizuri wananuna . Upinzani Tanzania kwao ni kuiombea vibaya Serikali ishindwe kuleta maendeleo.

Wana siasa sio watu wema. Angalia wanavuowaletea wenzao majanga
 
Alafu kuna watu wanasema vibaka na mteja hawaogopi kufa! Mbona battery haijachomolewa hapo?
 
Hili suala la wafanyabiashara ndogo ndogo kukaa maenea ambayo siyo lifanyiwe kazi, juzi nimesogea pale ukumbi wa mikutano wa nyerere walipohamishiwa Tanroads napo mama ntilie wameshaweka vibanda mambo hovyo hovyo tuu
 
Wakati wa awamu ya nne serikali hasa wizara ya ujenzi ili simamia sheria ya kulinda miundo mbinu ya barabara kwa kutoruhusu biashara, magari na hat a vibanda vya biashara kufanyika, kuegeshwa au kujegwa pembeni ya barabara, Kwenye service road na hata Kwenye njia za watembea kwa miguu.....

La ajabu Yule yule alitekuwa abomolea watu vibanda baada ya kupata madaraka ya juu ya nchi amehalalisha biashara kufanyika biashara kwenye barabara kiasi kwamba barabara na mitaa mijini imegeuka kuwa masoko bubu... AJILI HII YA MLIMANI CITY IWE FUNZO NA ISHARA KWA VIONGOZI YAKUWA KUNA JANGA WANALIPALILIA
 
]Sasa hiyo si ajali na sio kawaida? Kwa hiyo watu waache kupanda gari kwa sababu yakipinduka wanakufa?
 
Majina yao kina nani?
Je ndugu wamejitokeza kuwatambua?

Halafu kuna watz wengi wanatembea bila vitambulisho huwezi amini!
 
Wanyonge hawana hela ya kulipia frem mkuu, kodi ya mwezi mmoja tu ndio mtaji wote, halafu unatakiwa kulipia miezi 6, atawezaje?
Ni kweli hilo ni tatizo.
Sasa kuliko kwaanika barabarani na kukoswakoswa na magari bora mipango ifanywe sehemu za viosk mji mxima.
 
Back
Top Bottom