Ajali Mlimani City: Yadaiwa watu watatu wamefariki

Wafanyabiashara ndogo ndogo wamevamia sana barabara na ni hatari sana kwa maisha yao,mbona wakifanya sehemu za sokoni zilizotengwa watu wataenda tu bila wasiwasi? Siasa nyingine ni upuuzi.
Upinzani huwa wanawatumia hawa, hata boda boda, ni shida tupu.
 
Barabara zote zimefanywa masoko ! Mungu anatusitiri sana ! Na roho zao zipumzike kwa amani !! Mamlaka husika siku hizi zinafanya nini !?
Siasa ndio zimetufikisha hapo, kuruhusu maeneo ya hifadhi ya barabara kuwa masoko, na trafic walishalisema sana lakini hawana jinsi mzee baba ameshasema waachwe!! Na siku moja utasikia tamko kuwa ukiwagonga tu hao unafungwa maisha.
 
Pale Mbagala likija kutokea Tatizo kama ili tutakua na msiba wa Taifa
Itakuwa balaa!! Juzi tu maeneo ya kongowe roli liliacha njia likauvaa mti bahati nzuri hakukuwa na watu mida hiyo ilikuwa ni usiku sana!! Mwanasiasa hana huruma na maisha yako, hata umwambie nafanyia biashara juu ya nguzo za umeme mkubwa HT, lakini sitagusa nyaya atakwambia sawa tu, ilimradi kuwepo wewe pale atapata kura yako!!
 
Kwakweli Mungu atunusuru maana hali ni mbaya, km utabahatika Kupita maeneo ya Rangitatu Mbagala utashuhudia,yaani Raia wamepanga biashara zao barabara kabisa ! Mimi huwa najiuliza mamlaka husika hazioni mpk itokee ajali mbaya iitwe Msiba wa kitaifa ndio watazinduka?
Barabara zote zimefanywa masoko ! Mungu anatusitiri sana ! Na roho zao zipumzike kwa amani !! Mamlaka husika siku hizi zinafanya nini !?
 
Siku hzi madereva hakuna kabsa.. Si angelipandisha katikati ya lile gema?

Mie nina kanuni moja AJALI HAIKWEPEKI ILA kuna uwezekano wa Kupunguza Makali.. Kama ilitakiw wafe watu 20 bas watakufa wawili.. So Tuwe makini na Maamuzi pindi ajali inapokaribia kutokea
 
Hayo ndiyo madhara ya kuruhusu wamachinga kufanya biashara hovyo hovyo tena kando kando ya barabara
 
Pole waliokumbwa na matatizo, Bahati mbaya haina mwenyewe ila hawa wenye maroli nao wanakuaga speed sana ata maeneo ya mjini.
Toa ushenzi wako hapa... Mjinga kabisa.. wewe huoni barabara zote zimefanywa masoko na vibanda vya Wamachinga
 
Barabara zote zimefanywa masoko ! Mungu anatusitiri sana ! Na roho zao zipumzike kwa amani !! Mamlaka husika siku hizi zinafanya nini !?
Mamlaka zipi unauliza . Wakati Magufuli alitoa ruhusa watu wafanye biashara popote wanapotaka kasoro kwenye viunga vya ikulu nadhani
 
Jaman kuna ajali hapa Mliman City lorry la Mafuta limewabana watu kweny mtaro ina sikitisha sana. Daaaah Mungu awaepusha na kifo. Watu kama kawaida wamejana, wanataka kuiba mafuta. Polisi wanafanya kazi ya ziada kuwafukuza hawatoki.


Nimepita hapo kuna crane linainua hilo tanker ila nina mashaka makubwa na uwezo wa crane maana limechokachoka linainua na kuzidiwa uokoaji ni wa kusuasua sana
 
Habari Wakuu,

Nimepata taarifa ya ajali maeneo ya Mlimani City ambayo imetokana na lori kuacha njia na kuwazoa wafanyabiashara wanaouza bidhaa mbalimbali nje ya Mall ya Mlimani City.

Taarifa zinaeleza kuwa watu 3 wamefariki pale pale.

Naendelea kufuatilia na nitawajuza hapa.
Kwa habari nilipata hakuna marehemu ila kuna mahutiuti waliojeruhiwa vibaya
IMG_20191123_132404.jpeg
 
Kwakweli Mungu atunusuru maana hali ni mbaya, km utabahatika Kupita maeneo ya Rangitatu Mbagala utashuhudia,yaani Raia wamepanga biashara zao barabara kabisa ! Mimi huwa najiuliza mamlaka husika hazioni mpk itokee ajali mbaya iitwe Msiba wa kitaifa ndio watazinduka?
Lakini pia hicho ni kiashiria kwamba tunaishi kwenye nchi maskini au ya ulimwengu wa tatu
 
Pale Mbagala likija kutokea Tatizo kama ili tutakua na msiba wa Taifa
Barabara ya Msimbazi, Kariakoo pia, yaani wamachinga wameteka road reserve, watembea kwa miguu wanalazishwa kuchangia barabara pamoja na magari, maduka yote yamezingirwa na wamachinga. Yaani vurugu tupu.

Vv
 
Poleni mliofikwa na hayo, na pia ni muhimu tena swala la biashara za barabarani kuwa reviewed, wachuuzi wadogo wadogo waone haya madhara liwe somo, mamlaka ziangalie namna sahihi ya kufanya waingize vipato vyao katika hali salama.

mungu wenu alipo over-rule by-laws za halmashauri husika zinazokataza kufanya biashara barabarani (lengo likiwa kuzi-undermine zile zinazoongozwa na upinzani) si mlishangilia lakini? Leo imekuaje tena?
 
Tuliposema Jiwe anawatafutia kifo kuwaruhusu kufanya biashara kiholela tukaonekana wabaya...
 
Hivi kwanini tunaruhusu watu wafanye biashara hata kwenye maeneo ambayo ni wazi hakutakiwi liwe na biashara yoyote?
Tatizo ni wanasiasa, siku za nyuma Serikali iliwazuia wamachanga kufanya biashara sehemu zisizo ruhusiwa wapinzani wakaja juu kuwatetea na kuwatumia kwenye kila maandamano ya kupinga Serikali huku wakiaminishwa kuwa wanaonewa. Serikali baada ya kuona wapinzani wanawatumia wamachinga kisiasa pale wanapozuiwa na Serikali kufanya biashara sehemu zisizo ruhusiwa, Serikali ikaamua kuwaruhusu wafanye biashara kwa uhuru na ndipo wapinzani wakakosa watu wa kuwaunga mkono wanapoitisha maandamano. Tatizo la siasa za nchi hii ni za kubomoa siyo kujenga ndiyo maana serkali ikifanya vibaya wapinzani wanashangilia na ikifanya vizuri wananuna . Upinzani Tanzania kwao ni kuiombea vibaya Serikali ishindwe kuleta maendeleo.
 
Back
Top Bottom