Ajali Mkoani Tanga; Watu 6 wafariki na 21 Majeruhi

Tanga! Kunani paleeeee eeeee mbona kila kitu kinakufa.....! Poleni sana ndugu zangu
 
Desember.... :(
Poleni wafiwa... Mwenyenzi awasaidie majeruhi waweze kupona na kurejea kwenye majukumu yao.
 
pole kwa wafiwa,majeruhi tunawaombea mpone haraka,mungu awasimamie ktk uponyaji wenu
 
kweli huu ni mwezi wa 12.....!? kwahalaka halaka hii itakuwa ajali ya 40 kama sijakosea,sina uhakika wangapi wamekufa kwenye ajali za mabasi...... innallilah wa innallilah lahjun.
 
Huu mwezi nadhani zaidi 50 wamezikwa kwenye haya magari na bado hakuna hatua wala tamko wakati akifa tembo mmoja lazma tamko litolewe
 
WATU sita wamefariki papo hapo na zaidi ya 12 kujeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya Toyota Hiace kuligonga kwa nyuma lori la mizigo lililokuwa limeharibika barabarani bila kuonyesha ishara yoyote eneo la Kange jirani na mizani mkoani Tanga!

Baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa Tanga kwa matibabu!
 
● Hivi eneo la Mkoa wa Tanga kunani?
Maana Maisha ya watu wengi Yanapotelea Mkoa huu ●
 
Mmmh! naona wenye magari nao wako bize kukamilisha mahesabu mwisho wa mwaka,Mungu atusaidie tu,R.I.P kwa marehemu wote,kwa majeruhi Mungu awashushie uponyaji Ameen
 
mdereva kuweni makini. acheni kukimbizana na pesa, Naamini ndo chanzo kikubwa cha ajali.
 
Back
Top Bottom