Ajali Mkoani Tanga; Watu 6 wafariki na 21 Majeruhi

M2flan

JF-Expert Member
Jun 27, 2013
414
250
Ni ajali iliyotekea hivi punde Mkoani Tanga katika eneo la Kange sehemu ya mizani ikiwa gari aina ya toyota hiace imegonga roli la mizigo kwa nyuma.

Majeruhi wamewaishwa hospitali ya Bombo.

Source: ITV
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,108
2,000
Tanga! Kunani paleeeee eeeee mbona kila kitu kinakufa.....! Poleni sana ndugu zangu
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,836
2,000
Desember.... :(
Poleni wafiwa... Mwenyenzi awasaidie majeruhi waweze kupona na kurejea kwenye majukumu yao.
 

andishile

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
1,430
1,225
pole kwa wafiwa,majeruhi tunawaombea mpone haraka,mungu awasimamie ktk uponyaji wenu
 

omary mwene

JF-Expert Member
Nov 6, 2013
293
0
kweli huu ni mwezi wa 12.....!? kwahalaka halaka hii itakuwa ajali ya 40 kama sijakosea,sina uhakika wangapi wamekufa kwenye ajali za mabasi...... innallilah wa innallilah lahjun.
 

Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
15,720
2,000
Huu mwezi nadhani zaidi 50 wamezikwa kwenye haya magari na bado hakuna hatua wala tamko wakati akifa tembo mmoja lazma tamko litolewe
 

DEMBA

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,244
2,000
mmmh kumekucha, jana mwanza leo tanga, hadi inatisha kwa kweli
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,455
2,000
WATU sita wamefariki papo hapo na zaidi ya 12 kujeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya Toyota Hiace kuligonga kwa nyuma lori la mizigo lililokuwa limeharibika barabarani bila kuonyesha ishara yoyote eneo la Kange jirani na mizani mkoani Tanga!

Baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa Tanga kwa matibabu!
 

Eligi

Senior Member
Mar 7, 2013
167
195
● Hivi eneo la Mkoa wa Tanga kunani?
Maana Maisha ya watu wengi Yanapotelea Mkoa huu ●
 

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,842
2,000
Mmmh! naona wenye magari nao wako bize kukamilisha mahesabu mwisho wa mwaka,Mungu atusaidie tu,R.I.P kwa marehemu wote,kwa majeruhi Mungu awashushie uponyaji Ameen
 

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,441
1,250
mdereva kuweni makini. acheni kukimbizana na pesa, Naamini ndo chanzo kikubwa cha ajali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom