Ajali mkoani Geita: Gari la RPC lawaka moto

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,910
2,000
Gari ya Kamanda wa polisi mkoa wa Geita na gari ndogo ya abiria aina ya Hiace leo mchana zimewaka moto na kuteketea baada ya ajali iliyosababishwa na dereva boda boda aliyekua amebeba mafuta ya dizeli.

Hata hivyo, Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Hendry Mwaibambe hakuwemo kwenye gari hiyo na amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imetokea leo majira ya saa 8.46 mchana katika eneo la Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.

Katika ajali hiyo, dereva wa boda boda ambaye inasemekana amepoteza maisha huku watu 16 wakijeruhiwa ambapo wawili kati yao ni askari polisi.

Akielezea tukio hilo, Kamanda Mwaibambe amesema dereva wa boda boda huyo alikuwa amebeba lita 100 za mafuta ya dizeli akaingia barabarani bila umakini na kugongwa na gari ya kamanda kisha kwenda kugonga hiace iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara na kusababisha magari yote kuwaka moto.

Amesema gari hiyo ya polisi yenye namba PT 4447 iliyokuwa ikiendeshwa na Koplo Manase Nestory imewaka moto kufuatia cheche za pikipiki baada ya ajali kuangukia mafuta yaliyomwagika.

Kwa mujibu wa kamanda, majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya ya Chato na kwamba hali ya dereva wa Hiace ni mbaya huku polisi wakitibiwa na kuruhusiwa kuondoka.

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,685
2,000
Bodaboda amebeba LITA 100 za Dizeli.. (Wamejuaje kama ni Lita 100 wakati wamesema zimemwagika??)

Hafu Hivi Lita 100 si ndoo 5. Unabebaje kwenye Bodaboda?

Na me sio mtaalamu ila je Dizeli nayo inawaka kama Petroli? Maana kwa hayo maelezo yanaonesha moto umesababishwa na cheche kisha cheche zikashika moto kutokana na wese (dizeli) iliomwagika.

RIP bodaboda.
 
Pyaar

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
14,820

Nimejaribu pia kufikiria sana juu ya ubebwaji wa hizo lita 100 kwenye boda boda. Kwa maana ya madumu matano @20 lts.
 
alubati

JF-Expert Member
May 29, 2016
3,563
2,000
Nimejaribu pia kufikiria sana juu ya ubebwaji wa hizo lita 100 kwenye boda boda. Kwa maana ya madumu matano @20 lts.
Mbona mwanangu wa miaka 12 anabeba madumu matano ya maji kwa baiskeli?,nyie watu wa wapi?
 
IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
9,751
2,000
Bodaboda amebeba LITA 100 za Dizeli.. (Wamejuaje kama ni Lita 100 wakati wamesema zimemwagika??)

Hafu Hivi Lita 100 si ndoo 5. Unabebaje kwenye Bodaboda?

Na me sio mtaalamu ila je Dizeli nayo inawaka kama Petroli? Maana kwa hayo maelezo yanaonesha moto umesababishwa na cheche kisha cheche zikashika moto kutokana na wese (dizeli) iliomwagika.

RIP bodaboda.
Wanabeba mkuu, wanafunga na kamba dumu 2 kila upande zinaninginia na moja pale juu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom