AJALI: Mbunge Paulina anusurika kifo, alazwa ICU na ziara yaahirishwa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Paulina Gekul, amenusurika kifo baada ya gari lake aina ya Harrier namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya, ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa Naibu Waziri wa Mazingira Luhaga Mpina Wilayani Babati Mkoa wa Manyara
0ead885e1c8321eed21c3646838024bc.jpg
Baada ya ajali hii kutokea mbunge Paulina Gekul alikimbizwa hospitali ya Mkoa wa Manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hicho na Madaktari ambao wanaomuhudumia mbunge huyo kulazimika kumsubiri Naibu Waziri ambaye aliingia kumuona mbunge Gekul

Hata hivyo baada ya ajali kutokea Naibu Waziri wa Mazingira akalazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa Babati huku Mpina akiipongeza Halmashauri ya mji wa Babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza Mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwa ajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.

Chanzo: ChannelTen
 
Pole sana Kwan Mh. Mbunge. Naamini Mwenyezi Mungu atamjalia aweze kupata nafuu haraka.

Ila inasikitisha sana kwani ajali zinazohusisha magari ya Wah. Wabunge zimeongezeka....!
 
Hivi ikitokea la kutokea tume ya uchaguzi wanazo pesa za kurudia uchaguzi kweli? maana walirudisha pesa kwa jamaa
 
Pole sana kamanda.. Lakini why harrier.. Hiz gari zichunguzwe.. Kuna uwezekano hatuzitumii itakiwavyo
 
Back
Top Bottom