Ajali mbaya zaidi zilitokea Tanzania, je serikali imechukua hatua gani zisitokee tena?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,799
1. Mv. Bukoba
2. Ajali ya treni iliyoshindwa kupanda mlima, ikarudi nyuma (Dodoma)
3. Air Msae
4. No Challenge
na nyingine nyingi.
 
Kuna ajali nyingine ilitokea Tukuyu Mbeya, kijiji kizima kilijaa misiba, watu waliteketea kwa moto walipokuwa wanajaribu kuiba mafuta kutoka kwenye gari la kubeba mafuta lililokuwa limepinduka
 
daaah nimekumbuka ajali ya trni dodoma na nyingine ni ile ya basi la mohamed trans lililoungua moto
 
Serikali inalawama lakini wananchi ndio wa kulaumiwa zaidi, gari imejaa na hamna siti unapanda. Dereva anakimbiza mko watu 50 mnamsubiri traffic akamate, mikanda hamfungi, gari bovu mnapanda. Konda anawapanga watano watano mnapangika tena serikali ifanye nini?

Dereva analewa manmuona mnakaa kimya, taka ziko nje ya mlango wako mnataka serikali ije itoe, utumii dawa ya penzi lawama unaitupia serikali.
 
ajali nyingine imetokea jana usiku huko mlima nyoka, mbeya. Chanzo ni mwendo kasi
 
Na sasa MV Spice!

Kinachoshangaza zaidi ni kujirudiarudia kwa majanga yanayofana...
1. Kuzama kwa MV Bukoba (Μei 1996)
2. Ajali za Treni Dodoma ( Machi 2009)
3. Kulipuka kwa Mabomu Mbagala (April 2009)
4. Ajali za Treni Dodoma ( Julai 2009)
5. Kulipuka kwa Mabomu Gongo la Mboto (Februari 2011)
6. Kuzama kwa MV SPICE (Septemba 2011)

Ewe Mola wetu, Uwalaze pema ndugu zetu waliopoteza maisha katika majanga haya, amina.
 
Back
Top Bottom