Ajali mbaya yatokea, Scania yagongana na Fuso Rwamishenye bukoba, imeua

instanbul

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
11,828
16,266
Ajali mbaya iliosisha gari aina ya scania kugongana uso kwa uso na fuso lenye mchele na dereva bodaboda imetokea Leo asubuhi maeneo ya rwamishemye karibu na stendi barabara kuu iendayo Uganda.katika ajali hiyo bodaboda alikuwa akipita eneo hilo wakati magari yakigongana na kupelekea magari hayo kumgonga na kusababisha kifo chake.huku madereva Wa magari hayo wakiumia.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi

==========

Ajali iliyohusisha magari mawili yatokea maeneo ya Rwamishenye (Kwa Kagambo) mjini Bukoba ,watu wanusurika...

Mashuhuda wamesema ajali hii imetokea asubuhi ya leo baada ya Lori aina ya Semi kukatika breki na kuivaa Gari aini ya Fuso kwa nyuma

Dreva wa Semi ilimladhimu kufanya hivyo baada ya kugundua mbele yake kuna Basi la Bunda lililokuwa likitokea stendi kuu ya Bk kuelekea Mwanza hivyo akafanya maamuzi yaliyo onekana ni salama kwake kuepuka kugongana na Basi hilo
13626362_737785829696901_425946105429358735_n.jpg

Gari hiyo aina ya Fuso yenye nambari T 920 BHW ilikuwa imepakia Mchele na Semi yenye nambari 789 BHW ikiwa na bidhaa mbalimbali mmoja aliyekuwa na pikipiki amejeruhiwa katika tukio hilo lililotoka mapema ya leo jumatano July 13 .

Updates;

Mwendesha bodaboda katika manispaa ya Bukoba Kabeya Furgence amepoteza maisha baada ya pikipiki yake aliyokuwa akiiendesha kufunikwa na gari aina Fuso yenye usajili namba T.620 AWT lililopinduka baada ya kugongwa kwa nyuma na gari aina Scania yenye usajili nambaT 789 DDV iliyokosa mwelekeo baada ya breki zake kukatika ambayo nayo ilipinduka pia.

Marehemu huyo alikuwa akiendesha pikipiki aina ya TVS star yenye namba za usajiliT 270 EGM na amefia katika hospitali ya mkoa wa Kagera,katika ajali hiyo watu wanne wamejeruhiwa na baadhi yao wanaendelea kupatiwa matibabu.

59213a179982cf2cf8ba2556b09782d0.jpg
 
Mwendesha bodaboda katika manispaa ya Bukoba Kabeya Furgence amepoteza maisha baada ya pikipiki yake aliyokuwa akiiendesha kufunikwa na gari aina Fuso yenye usajili namba T.620 AWT lililopinduka baada ya kugongwa kwa nyuma na gari aina Scania yenye usajili nambaT 789 DDV iliyokosa mwelekeo baada ya breki zake kukatika ambayo nayo ilipinduka pia.

Maheremu huyo alikuwa akiendesha pikipiki aina ya TVS star yenye namba za usajiliT 270 EGM na amefia katika hospitali ya mkoa wa Kagera,katika ajali hiyo watu wanne wamejeruhiwa na baadhi yao wanaendelea kupatiwa matibabu.

Chanzo: ITV
 
R.I.P
 
Kuna haja ya kurudia mila zetu ili tuanze kutambika maana ajali hizi zimekuwa nyingi muno huenda mizimu ya babu zetu imekasirika
 
Eeeh Mola tunusuru..
Mana naona sasa ni msimu wa ajal za kufeli breki, haya ndo yale yale yalotokea mbalizi..
R.I.P MR BODABODA
 
Back
Top Bottom