Ajali mbaya ya uso kwa uso kati ya Bus na lorry mchana huu!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,219
Ajali mbaya imetokea muda huu kati ya basi ya abiria la Ally Bus Service lililokuwa linatoka Bariadi kwenda Mwanza lilipogongana uso kwa uso na lori la mzigo maeneo ya malampaka na kwa bahati nzuri hakuna watu waliopoteza maisha na majeruhi wamepelekwa kwenye hosptal ya Maswa.

Source: Crashwise akiwa eneo la tukio!
 
Na mdau wetu aliyekuwa eneo la 2kio amepata kuongea na dereva wa lori na driver wa lori akesema hawakuwa speed sana hata watu walioumia ni kwa kujigonga ama wenyewe kwa wenye au kwenye viti kutokana na kutokufunga mikanda..........na aliongeza akasema kulikuwa na gari lilimpita kwa kasi na kutimua vumbi kubwa hali iliyompelekea kutoona mbele kwa mbali na ndipo ghafla akaliona bus la Ally na katika harakati ya kutaka kukwepana wakajikuta wanagongana uso kwa uso.........!!

Na tumshukuru MUNGU wa rehema hakuna mtu aliyepoteza maisha!
 
huyo tajiri wa Ally's lazima achanganyikiwe...ni mwezi jana tu gari lake lilipinduka kwenye ile ajali iliyojumuisha magari mabasi matatu
 
Nikiwa anasafiri kwenda kanda ya ziwa, kama nataka nifike mapema huwa napanda basi la Ally's. linakimbia sana ila uzuri wake madereva wake wana uzoefu mkubwa.
 
Mtu anapata ajali au majeraha yatokanayo na jambo la bahati mbaya unamuita MUHANGA! Si dhihaka hiyo?

Hao ni waathirika, tubadilike.
 
Back
Top Bottom