Ajali mbaya ya Jet Fighter uwanja wa ndege Dar, tumempoteza kamanda mmoja

Amekufa kwa ajili yetu Watanzania sote. RIP Kipenzi chetu na Asante

Amekufa kwa ajili yetu???!!! Ina maana singekufa yeye sisi ndio tungekufa??? Please, usinijumlishe mimi, familia yangu, ukoo wangu, kabila langu na Watanzania wenzangu katika hili!
 
umeona eeee Remote??! neno la kishariii? yaani wa visiwani wamenipa tabasamu kwa mwaka huu!
dear cacico yani mwezako nikiwa na stress zangu tu huwa naingia FB kwnye page ya uamsho.. Nkliona hlo neno tu stress zooote kwsha; asante kwa uamsho kuongeza cku zangu za kuishi
 
Last edited by a moderator:
amka2.gif
MWANAJESHI mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya ndege ya mafunzo waliyokuwa wamepanda maofisa wa Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ) kupoteza mwelekeo na kuanguka katika eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.
Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali Kapambala Mgawe, alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa haijaruka, lakini maelezo yake yameonekana kujichanganya.
Alisema wakati ndege hiyo ikijiandaa kuruka ikiwa na maofisa wa mafunzo wawili, ilipoteza mwelekeo na kuserereka na kuelekea ndani kwenye hanga kitendo kilichowafanya waamue kujinusuru maisha yao.
"Ndani ya hanga hilo kulikuwa na ndege nyingine mbili, lakini hata hivyo tunashukuru hakuna madhara yaliyotokea, kila kitu kiko salama," alisema Kanali Mgawe.
Alisema wanajeshi hao, kila mmoja aliamua kuchumpa kwa mwamvuli ambapo Kapteni Magushi alianguka juu ya paa la jengo lililokuwa karibu na eneo hilo ndipo alipopoteza maisha.
Alimtaja mwanajeshi aliyenusurika katika tukio hilo, kuwa ni Kapteni Kwidika, ambaye amekimbizwa katika hospitali ya kijeshi Lugalo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wanajeshi hao walikuwa katika shughuli zao za mafunzo ya kawaida.


Source : Tanzania Daima
 
Huu uzi uwekeni sawa sawia hiyo Jet ilikuwa ina paa au ilikuwa inatua... Majibu Utata Sana haya wewe Myahudi Moshe Dayan na Gama
 
Last edited by a moderator:
"Ndani ya hanga hilo kulikuwa na ndege nyingine mbili, lakini hata hivyo tunashukuru hakuna madhara yaliyotokea, kila kitu kiko salama," alisema Kanali Mgawe.
Watanzania lugha yetu inatupa tabu sana, hususan mawasiliano ya umma. Jamii imefikwa na maafa, mtu kafa, mwingine yuko hospitali, wewe unaenda kutoa statement yenye maneno "tunashukuru hakuna madhara yaliyotokea, kila kitu kiko salama"!

Kanali mzima! Sijui ni elimu yetu msingi wake mbovu au ni kwa vile wazee wengi hawa Kiswahili sio lugha yao ya asili?


 
Poleni sana wana anga wetu na walinzi wetu wa anga letu,naomba kuwakumbusha kuwa hizo ndege hazina mwisho wa kuruka?maana ni zamani sana,mnatakiwa kuomba kuhakikishiwa usalama wenu na wanaozitengeeneza na waje mara kwa mara au waje wachache kuwa nanyi kwa ukaguzi wa mara kwa mara.....hizo ndege za mafunzo mara 2 ndani miaka 2 kuua marubani,hata ile ajali ya msata nayo ni ya mafunzo
 
Kwli inasikitisha sana Tena naionea huruma Familia ya huyo mwanajeshi aliyepoteza uhai kwani kibongo bongo haitakumbukwa tena.
 
Nchi hii iko pesa mingi wewe...sisi tumejiandaa vema kijeshi na kivifaa....kunaukweli kwenye hii kauli iliyotolewa na mkubwa flan
 
RIP kepteni Deo Magushi.

Nimetoka kuangalia picha yake niliyopiga naye pamoja na wana-Pugu wengine mwaka 1998. Nakumbuka nilimwacha Pugu sekondari akiwa form five mwaka 1998. Bahati mbaya siwezi kuiweka picha humu kwa sababu ina watu wengine ambao ni member humu. Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom