Ajali mbaya tena huko Mkoani Morogoro! Watu 4 wafariki hapo hapo!!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,219
Katika hali inayoelekea kuwa desturi ya hapa Nchini kwetu ni kwamba ajali mbaya imetokea leo huko Kilombero Mkoani Morogoro na watu wa4 wakapoteza maisha hapo hapo! MUNGU tunusuru na ajali hizi za kutwa!

Na wote wale waliofikwa na msiba MUNGU awajaze nguvu katika kipindi hiki kigumu! Na marehemu wote MUNGU awalaze mahala pema peponi!

Source ni ITV
 
Poleni sana kwa ajili,waliofariki mungu aziweke roho zao mahali pema peponi!
 
Chanzo cha ajali kinasema ajali ni mwendo kasi na pamoja na kupoteza uhai wa watu wa4 hata hivyo majeruhi zaidi ya nane wamelazwa na hali zao zinaendelea vema! Ajali imehusisha gari aina ya Isuzu pikup.
 
Hii ajali imetokea maeneo gani ? Na gari aina zimehusika, Maana pale ruaha(kilombero) mpaka mikumi mizani kuna usafiri wa Noah, hizo noah zenyewe zinajazwa noma, halaf iyo spidi aibu, siku 1 nilipanda nilijuta nikawa namuomb mungu aepushe, ingetokea ajali cjui kama kuna mtu angetoka, tulijazwa km embe maana pale mbele tulibanwa 3 na dereva wa 4, kinoah unavyokijua tuliingia watu 19, halaf spidi ikipungua 120, dereva mwenyewe ukimuangalia hana uzoefu hata wa mwaka.
 
Poleni sana wafiwa wote na wote mlioathirika kwa namna yoyote na ajali hiyo.R.I.P marehemu wote.
 
hapo umeeleweka baada ya kueleza chanzo cha ajali na pia ajali imehusisha magari yepi sio pale mwanzo ulikuwa na haraka utafikiri unaoga nje
 
Back
Top Bottom