Ajali mbaya stendi ya Mbezi

keizerjohn

Senior Member
May 12, 2013
113
13
Nilikuwa natoka mazoezini jioni ya leo, muda Wa saa mbili kamili hivi usiku huu, nilipofika stand kuu ya mbezi nilivuka barabara kuingia stand tokea upande wa pili. Kulikuwa Na foleni ndefu ya Magari yaendayo ktkt ya mji.

Kuna kijana mmoja naye alikuwa anavuka, kumbe Basi la Superfeo kutoka Songea, lilikuwa limetanua kulia kujifanya kuwahi kuliko wengine. Gari la kulia lilimruhusu kijana, alipovuka Gari hilo aliangalia kushoto akaona kweupe, kumbe Basi hilo limetanua kulia, basi kishindo kikubwa kilisikika akatushwa juu Na kutua chini. Tulipomfunua tulishuhudia damu nzito zikibubujika kila upande wa kichwa.

Basi lilifunga breki kisha likaondoka kwa kuendelea kutanua lkn kufika njia panda ya kwenda Kinuerezi likakutana USO kwa uso na magari yanayopandisha mikoani likawa blocked na wasamaria wema wakalizingira.

Mtu katoka Songea Salama km zaidi ya 1000 amebakiza km 20 anatanua hovyo na kuua!

Madereva muwe makini
 
Nilikuwa natoka mazoezini jioni ya leo, muda Wa saa mbili kamili hivi usiku huu, nilipofika stand kuu ya mbezi nilivuka barabara kuingia stand tokea upande wa pili. Kulikuwa Na foleni ndefu ya Magari yaendayo ktkt ya mji. Kuna kijama mmoja naye alikuwa anavuka, kumbe Basi la Superfeo kutoka Songea, lilikuwa limetanua kulia kujifanya kuwahi kuliko wengine. Gari la kulia lilimruhusu kijana, alipovuka Gari hilo aliangalia kushoto akaona kweupe, ikumbe Basi hilo alikuwa anaangalia kushoto

Baada ya hapo nini kikatokea?
 
unakimbilia wapi andika kinachoeleweka we sema superfeo imemgonga ... sio stori ndefu ujumbe wa mistari miwili.
 
Basi limekamatwa lipo Kituoni na ule mwili ulibebwa. Sijajua Kama yu hai hadi ripoti ya daktari, lakini kwa maacho nilimuona kapoa maana damu zilikuwa nzito zimetapakaa na alikuwa amebonyea kichwani, kapoa kbs
 
unakimbilia wapi andika kinachoeleweka we sema superfeo imemgonga ... sio stori ndefu ujumbe wa mistari miwili.

Bora ujue chanzo cha ajali ili ujifunze yasije yakakukuta wewe kesho, samahani lkn. Ndio maana nikawa detailed maana haidaidii kusema Basi limeua, Bali limeuaje sivyo!! Acha haraka
 
Back
Top Bottom