Ajali mbaya imetokea Morogoro road,wazungu wa 3 wamekufa.

CHIPANJE

JF-Expert Member
May 1, 2011
321
53
Kuna ndg yangu anasafiri kuja Dodoma,amenijulisha kua kuna ajali mbaya imetokea scania mbili zimegongana.Nasikia gari ya pick up ya wazungu imejibamiza ikiwa haijatii amri ya kusimama na kwenda kuovateki na kugonga hiyo scania ilionguka.

Inasemekana wazungu wa 3 wamekufa na mwingine amekimbizwa Tumbi akiwa amepasuka kichwa.

Na hadi hivi sasa kuna road block katika barabara hiyo,hivyo hakuna gari zinazokwenda Dar wala Dom.

Mwenye taarifa nzuri atujuze tafadhali.
 
RIP wazungu 3! Huenda walikuwa wanakwenda kwenye exploration ya madini ya Ruby maskini.
 
RIP wadhungu! Hawakusimama kwakuwa walikuwa na mali za magendo na dhahabu zetu! Sachini mabegi hayo mtajua ukweli!
 
Jamani wazungu, RIP! Vipi wabongo wetu, madereva wa scania wamepona?
 
Dah ajali ajali kila kona ya tz, MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU WAZUNGU MAHALI PEMA PEPONI
 
Ninachokiona hpo ni kuwa wazungu 3 hawakiweza kutambua zile ishara zetu za kuweka majani barabarani na hii huwa inawacost foreigners wengi sana kwenye hizi highway zetu...hivi kale kasheria kakutotumia majani kama ishara hakajaanza kufanya kazi eeeh!?..nway R.I.P wazungu 3
 
Back
Top Bottom