kakuruvi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2009
- 770
- 256
Jamani!!!! Mungu atufumbue akili tupate njia muafaka kudhibiti ajali hizi.
Leka
Mungu ni mwema tu, kuna ajali lakini nyingi tunajitakia madereva wengi hawajui sheria za barabara na kama wanazijua wanapuuza.
-Dereva anaovertake kwenye kilima au kwenye kona unatarajia nini?
-Matairi ya gari ni vipara unatarajia nini?
-Askari anaacha kumtoza faini mkosaji barabarani faini 250,000 anapozwa 5,000 anamwachia aende, wataacha makosa kweli? unatarajia nini?
-Dereva anaongea na simu gari iko mwendo unatarajia nini?
-Dereva amelewa unatazamia nini?
-Uwezo wa gari tani 3 imebeba tani 3.750 unatarajia nini?
Mungu awarehemu waliopoteza maisha na majeruhi wapone upesi. Inshaalah!