Ajali Mbaya Chalinze: Zaidi ya 20 Wapoteza maisha papo kwa papo!

Omumura

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
476
18
Kuna habari kwamba mchana huu katika eneo la kitumbi Mkoani Tanga kumetokea ajali mbaya ikihusisha basi la chatco lililokuwa likitokea Dar pamoja na Fuso, vifo vipo pamoja na majeruhi,tunaendelea kufuatilia zaidi ukweli wake!!
 
Kumetokea ajali mbaya iliyohusisha basi la Chatco na Basi jingine dogo eneo mbele ya Chalinze.

Kwa mujibu wa Radio One Breaking news, Frank Mchaki amehijiwa live, amesema ameshuhudia miili 16 ikiopolewa toka kwenye basi la Chatco na miili 4 toka kwenye basi dogo.

Update zitafuata.

NB. Idadi ya vifo inaweza kupungua au kuongezeka, kufuatia baadhi wa waliozaniwa kufa, kukutwa walizimia, ama waliojeruhiwa, kuzidiwa na kuongeza idadi.

Ajali ni ajali, pole kwa wafiwa, na ehueni kwa majuruhi.
 
Ohhhh my God,Mungu uturehemu.Wakati wenzetu nchi nyingine wanamalizwa na matetemeko na matsunami.sisi ajali zinatupotezea nguvu kazi.
Poleni watanzania sababu inawezekana ndugu yako ni victim.
 
Poleni watanzania kwa kufikwa na majanga ya ajali every time. RIP wote waliowahi kwa muumba, na majeruhi Mungu awarehemu mpone haraka.
 
Wanao wamaliza wale kwa matetemeko ya ardhi, ndio hao hao wanao tumaliza kwa ajali Tanzania na kwingineko duniani.Laiti tungezinduka,tungepona.Vinginevyo tutaendelea kuteketea.

Ohhhh my God,Mungu uturehemu.Wakati wenzetu nchi nyingine wanamalizwa na matetemeko na matsunami.sisi ajali zinatupotezea nguvu kazi.
Poleni watanzania sababu inawezekana ndugu yako ni victim.
 
Poleni wafiwa,
mungu awatie nguvu wahusika wote katika kipindi hiki kigumu

roho za marehemu zipumzike kwa amani,Amina
 
mungu aziweke roho za marehemu mahali pema, na awape faraja majeruhi wote wapate nafuu haraka
 
Kuna habari kwamba mchana huu katika eneo la kitumbi Mkoani Tanga kumetokea ajali mbaya ikihusisha basi la chatco lililokuwa likitokea Dar pamoja na Fuso, vifo vipo pamoja na majeruhi,tunaendelea kufuatilia zaidi ukweli wake!!
Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu

roho za marehemu zipumzike kwa amani amina
 
Kwa kweli inaumiza sana inapofika wakati huoni juhudi zozote za mamlaka zinazohusika na usafirishaji katika kupunguza ajali barabarani. Hayo mabasi mengi yake utakuta ni mwendo kasi tu basi. Basi linapelekwa mbio sijui dereva anakuwa tahadhari gani endapo kunatokea tatizo. Na hizi rushwa kwa askari wa trafiki zinachangia kwenye hili tatizo...Poleni sana mliopoteza wapendwa wenu na wale walioumia ajalini...
 
ndo kusema ni ajali mbili tofauti au? maana naona kuna moja imetokea chalinze kati ya basi na gari ndogo, na ingine tanga kati ya fuso na basi. which is which?
 
Barabara Barabara!
Bila ya serikali kusema enugh is enough na kuinvest kwenye barabara hatutaondoa ajali ambazo zinaweza kuondolewa.

Bado Tanzania tuna single lane kwenye barabara nyingi kuu ziendazo masafa marefu.
Assume tuna double lane oneway ,hakuna kupishana kwenye the same lane ,tungepunguza ajali .
 
Again? Oh my Lord!

Jana si kulikuwa kunafanyika ukaguzi wa Mabasi pale Kituo cha Mabasi Ubungo?

Kuna tatizo somewehre for real!

Poleni wote
 
jamani madereva mbona mnatumaliza -
chanzo lazima ilikuwa mwendo kasi
Mungu aziweke roho za marehemu pema peponi pia majeruhi awajaaalie kupona haraka
 
Back
Top Bottom