Ajali lori laning’inia ‘Daraja Mfugale’- jijini Melbourne, Australia

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
46,918
122,177
LORI linalosafirisha bidhaa za mayai na nyama ya kuku nchini Australia, limepata ajali na kubaki limening'inia kwenye daraja juu ya mithili ya lile la Mfugale, jijini Dar es Salaam, eneo la Tazara.

Taarifa za mtandao juzi jioni zinasema, bidhaa zilizokuwa zinasafirishwa na lori hilo zilimwagika na kutapakaa kwenye barabara iliyoko chini na inaelezwa dereva wa lori hilo alijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Hata hivyo, kuna taarifa dereva huyo hakujeruhiwa katika hali mbaya zaidi, ingawaje alipata ajali katika mazingira ya hatari zaidi dhidi ya maisha yake, ikilinganishwa na eneo lilikopatikana ajali hiyo.

Inaelezwa kwamba, tayari uchunguzi ulishaanza juzi hiyo jioni kubaini chanzo cha ajali, ingawaje kuna taarifa zisizo rasmi kwamba, lori hilo liligonga kizuizi pembeni mwa barabara na kupinduka.

Eneo la juu ambako gari hilo lilipata ajali, ni mithili ya darala la Mfugale katika eneo la juu inakopita barabara ya Nyerere na mizigo iliangukia mithili ya barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam, mazingira yanayofungua somo la uangalifu kwa watumiaji wa Darala la Mfugale ambalo bado ni jipya na limezinduliwa siku chache zilizopita.

Source: IPP Media.
IMG-20181122-WA0000.jpeg
 
Ngoja nikiwa narudi home leo ntapiga picha maandishi pale upande wa kutokea Airport iliuamini maandishi mku tumelize ubishi. .

Ohoooo, ok ntapiga kiujanja ujanja nisije nikangojwa pale.
Kikubwa uwe muangalifu mkuu, uchukue selfie ya kiumaridadi kabisa.

Ikiwezekana iwe kama ya SISI Tv kabisa
 
Ingekua habari njema kwetu CHADEMA
Mmetamani ajali na mtazipata nyingi tu kwenu na vizazi vyenu walahi
Ili mfurahi zaidi watu wa karibu yenu na watoto wakipuputika walahi na iwe hivyo milele walahi
 
Kikubwa uwe muangalifu mkuu, uchukue selfie ya kiumaridadi kabisa.
Kuwa makini kuna mahali haparuhusiwi kupiga picha mfano kivukoni, ndani ya kivuko n.k. Kuna alama kabisa usipige picha...sasa wewe kuwa mkaidi uone kitakachotokea. Nakuhakikishia salamu ya 'Salamaleko utaitikia tumsifu milele amina !' bila kujua.
 
Kuwa makini kuna mahali haparuhusiwi kupiga picha mfano kivukoni, ndani ya kivuko n.k. Kuna alama kabisa usipige picha...sasa wewe kuwa mkaidi uone kitakachotokea. Nakuhakikishia salamu ya 'Salamaleko utaitikia tumsifu milele amina !' bila kujua.
Ahsante kwa kusisitiza nilichokisema
 
Back
Top Bottom