Ajali kwenye mashindano ya rally yasababisha kifo na majeruhi Tanga

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,471
4,424
Ajali kwenye mbio za magari yaliyokuwa yanafanyika Tanga yameacha majeruhi 4 waliovunjika mguu na kifo cha kijana mmoja.Huku binti mmoja akinusurika baada ya gari kuruka na kupaa juu yake

Dereva la moja ya gari iliyokuwa inashindana alikuwa kwenye spidi kali ku cover muda aliopoteza kurekebisha gari ndipo aliposhindwa kuhimili corner na kuvamia mashabiki.

Mungu awaponye kuna michezo sio ya kuwa kimbele mbele kuangalia kama rally
 
Hawa jamaa bana huwa wanakaa barabarani kabisa wakijisahau kwamba hilo ni chuma tu muda wowote linaweza kufanya yake ...R.I.P kwa aliye tangulia na wapone haraka majeruhi

Hivi safety officers walikuwepo kweli ? Inasikitisha na hongera pia kwa Pandya kwa kutoboa namba moja
 
Kwenye video hapo Michael maluwe anasema Traffic walikuwepo na ambulance pamoja na watu wa Huduma ya kwanza

Traffic waliwaambia zaidi ya mara mbili watu waliokaa angle ilipotokea ajali hio watoke hio sehemu sio nzuri kukaa ila walikaidi..baada ya ajali waliwahishwa hospitali ya Mombo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom