Ajali, Kondoo: Basi la Kampuni ya Sharon Classic lateketea kwa moto maeneo ya Bicha

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Basi linalomilikiwa na kampuni ya Sharon Classic lililokuwa linatoka Moshi kuelekea Iringa, limeteketea kwa moto maeneo ya Bicha wilayani Kondoa.

Kwa taarifa za awali na shuhuda wa tukio hilo la ajali anasema abiria wote wametoka salama isipokuwa baadhi mizigo ilivyokuwa kwenye buti imeteketea huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa bado hakijafahamika mara moja.
IMG_20181119_161507_125.jpeg
IMG_20181119_161445_738.jpeg
 
Ni mkoa gani? maana mimi naijua Wilaya ya Kondoa iliyopo Idodomya (Dodoma), hiyo Kondoo ipo Mkoa gani?

Alafu hizi ajali za Moto mbona zimekuwa lukuki, labda kuna haja Askari/Wataalamu wa moto wawepo Barabarani sambamba na Trafiki, huenda wakikagua Bus wakaweza kung'amua viashiria vinavyoweza kusababisha moto na kuzuia majanga. na kuzuAttach filesia.
 
Nafikiri ni wakati sasa vyombo ya serikali vifanye uchunguzi wa mfumo wa umeme wa haya magari ya kichina tusingoje maafa au mpaka Rais aseme. Tamesa na Tbs wafanye kazi zao kuokoa maisha ya watanzania.
 
Taarifa ya ajali BM nimekucheki umepiga like halafu ukaondoka, nikawaza leo hajasema lolote

Mungu atunusuru na hizi ajali za moto

Mkuu ubarikwe sana kwa kufutilia habari, pamoja sana.
Nakukubali mzee wa taarifa za ajali.
Mungu ashukuriwe kwa kuwaokoa watu wake.
Mwaka huu makampuni ya bima yataisoma namba.
 
WaTanzania kama mbumbumbu vile error ndogo wataanza kuijadili na sio content ya habari.
Halafu mkuu niliweka Bicha ambapo angefahamu kuwa ni wilaya ya Kondoa.

Asante mkuu kwa kuwakumbusha
 
Back
Top Bottom