Ajali imetokea barabara ya Singida - Dodoma

Ili ufanye biashara ya malori lazima uwe na lori kuanzia tano na kuendelea..
Ili ufanye biashara ya mabasi makubwa lazima uwe nayo matano na kuendelea.

Basi likitembea 1000km likafika safari yake,kesho yake marufuku kutembea barabarani, lifanyiwe checkups na small repairs..

Mabasi yote na malori matairi yanunuliwe kwa authorized dealers walioizinishwa na serikali na tyres za kufungwa ziwe specified.

Gari zote za abiria na mizigo zinazosafiri mikoa tofauti tofauti lazima ziwe na pre-start books ambazo asubuhi dereva lazima acheki..kwa mabasi lazima isainiwe na mafundi wa kampuni husika inapoanzia safari kwa malori isainiwe na fundi wa kampuni mwanzo wa safari na huko njiani ni dereva...

Madereva wote wa malori na mabasi lazima wawe na minimum basic education ya form four..na kuwe na proffesional driving licences kwa madereva wa malori na mabasi tu baada ya kuhitimu na kutest...
Kila mwaka kuwe na licence certification kwa hawa madereva kutestiwa na update licence zao.

Udereva iwe kazi rasmi inayotambulika na serikali kwa madereva kuwa na mikataba, posho, medical insurances, leave kama waajiriwa wengine...

Jeshi la polisi liajili sasa vehicle inspectors well qualified na wawe trained kulingana na mahitaji...na hawa wawe wanafanya road patrol kwa ajili ya random checks kwenye mabus na malori hasa brake sytems, tyres, power trains, engines nk.....hizi ziwe zinafanyika barabarani hasa wakati wa kula mnavamia mnasample gari kadhaa, bus stands kubwa na wakati mwingine kuyaita baadhi ya mabus na malori kwenye Inspecton centers..

Makampuni ya malori na mabus yaanze sasa kuajili well qualified engineers wenye elimu, exposure na uzoefu unaohitajika kwa ajili ya management ya haya magari... Serikali iyakague haya makampuni kwenye ajira zake na watu inaowaajiri pamoja na mishahara kwa watu wao..

Tanroads waanze sasa kufanya road patrol za mara kwa mara pamoja na kuwa temporary road signs incase kuna fault mahala barabarani imetokea, kuwe na quick repair ya pits, mawimbi nk...wawe na link na jeshi la polisi pamoja na watumiaji wa barabara hasa mabus na malori kuwe na online daily breafing kwa mabus yote yanayokuwa barabarani kwa kila eneo kupata daily roads updates...

BILA KUFANYA HAYO TUTAKUWA KILA SIKU TUNAOKOTA MAITI , KUHARIBU BARABARA, KUHARIBU MALI, NA KUENDELEA KUKUZA JAMII MASIKINI.... tuache upumbavu na kuishi kama zama za mawe..
Umeeleza Inavyotakiwa kuwa Sasa Kuna Ilivyo ndugu
 
Madereva wa magar wakigongana huwa wanabamiza zaid upande wa abiria kama upo kushoto ya dereva wakat wa safar ile sehem inakuaga siyo salama hachelew kukuuzia kicheche, tanker imeharibika sana cabin lakin ukiangalia upande ulio haribika zaid n upande wa abiria kama kuna mtu alikua hapo nafikiri atakua na hali mbaya sana kama siyo kufariki kabisa
 
Katikati ya Bahi na Manyoni ni wapi?
Sijajua exactly location hata mtoa mada hapajui ila kwa kuangalia mazingira nikasema ni maeneo hayo con toka Manyoni to Singida miti kama hiho nichache sana yawezekana ikawa KINTINKU au popote
 
Kaka usiwalaumu madereva, kumbuka wana family na ndugu wanawowategemea!

Uzuri hii kampuni ya MOIL nina ndugu zangu wawili ni madereva, mmoja ni bamkubwa na mwingine mtoto wake wa kwanza naye dereva humo, Nikupe sababu ya kwanini hili kampuni hata gari zake ukisikia limepata ajari kosa sio la dereva.

Huyu tajiri wa MOIL Mansoor kwa sasa kamwachia mtoto wake ambae ni mbunge wa CCM wilaya ya kwimba anaitwa Shaniff, anamiliki zaidi ya tanks 100+ local na transit Africa mashariki yote.. Tatizo moja ana magari mengi IVECO nafikiri 90% ana Scania chache na DAYUN kaleta majuzi hivi tu, used hizi gari ni mbovu nyingi zina ugonjwa wa kuvuja upepo, kupasua busta na kuchemsha yaani zina tabia ya kuchemka na maji kuisha kwenye radiator haraka sana na zote hizo IVECO ni Automatic!

Mbaya zaidi gari ikipata hitirafu wakimwambia ashughulikie anawaambia wapaki kwanza wasubiri services ambayo hata kama ni tatizo dogo dereva anaweza kukaa mwezi mzima (imagine upo Dar familia ipo Mwanza maisha ya Dar gharama kulala, kula na huduma zingine ukae mwezi mzima unangoja services lazima pesa ukuishie mapema tu) so wengi wanaogopa kusema gari mbovu wanatembea nazo tu make gari hata ikiharibikia Mwanza tajiri anataka uende Dar unaikokota mpaka Kigamboni Deport ukapaki usubiri services hii nakwambia sabu imemtokea mzee mara kadhaa na mimi nikiwa niko nae safarini so nlkua najionea mwenyewe changamoto za kazi hii sio nakusimulia ya kusimuliwa.

Kilichonifanya nistuke hii ajari ni kua mpaka sasa mzee wangu anaendesha gari mbovu haishiki break na inapasua sana mipira ya upepo amepaki gari mara 2 Dar ku ngoja services ajabu ni kwamba MOIL anachokifanyaga ni ya kua anawaambia mafundi wa kampuni watoe spares kwenye gari mbovu zilizopark Deport palepale na kuhamisha kwenye gari ya matatizo ndiyo michezo yake..

Inshort gari nyingi za MOIL ni mbovu basi tu madereva wanafanya kazi katika mazingira magumu mno sometimes pesa zao za posho na mishahara ndiyo zinafanyia services gari za kampuni make wanajua tabia ya tajiri ni bahiri na hajari services za gari zake.
 
dah inasikitisha sana, alimchukua mdogo mdogo wake kwa nia njema kama sehemu ya ajira au naye baadaye aje kuwa dereva lakini ndio hivyo Mapenzi ya Mungu hamna namna..
Inasikitisha sana kaka..
 
Huyo wa Moil inaonekana alikuwa upande wake...huyo mwenye tela jekundu alikuwa ana overtake akajaa upande wa mwenzake.
 
Siku hizi adi wabeba mafuta wana ligi
Hmm! Labda kampuni zingine aisee sheria za barabarani zinatumika vilivyo kwa hawa usione hivyo bro, Wanapigwa faini za kufa mtu sabu ni hatari sana kumbuka wanatembea na mabomu roho mkononi. Wenye ligi ni wale wa Transit tu wanaoenda nchi jirani wao hata hawabanwi sana ila local transporters wanabanwa mno. Safari ya Dar to Mwanza tank anaweza tumia siku 2 na nusu njiani kwa kufata sheria kinyume cha hapo traffic wanasubiri wakupe risit tu uchangie pato kwa pesa zako za posho na mshahara, tajiri hata hausiki ani.
 
Ili ufanye biashara ya malori lazima uwe na lori kuanzia tano na kuendelea..
Ili ufanye biashara ya mabasi makubwa lazima uwe nayo matano na kuendelea.

Basi likitembea 1000km likafika safari yake,kesho yake marufuku kutembea barabarani, lifanyiwe checkups na small repairs..

Mabasi yote na malori matairi yanunuliwe kwa authorized dealers walioizinishwa na serikali na tyres za kufungwa ziwe specified.

Gari zote za abiria na mizigo zinazosafiri mikoa tofauti tofauti lazima ziwe na pre-start books ambazo asubuhi dereva lazima acheki..kwa mabasi lazima isainiwe na mafundi wa kampuni husika inapoanzia safari kwa malori isainiwe na fundi wa kampuni mwanzo wa safari na huko njiani ni dereva...

Madereva wote wa malori na mabasi lazima wawe na minimum basic education ya form four..na kuwe na proffesional driving licences kwa madereva wa malori na mabasi tu baada ya kuhitimu na kutest...
Kila mwaka kuwe na licence certification kwa hawa madereva kutestiwa na update licence zao.

Udereva iwe kazi rasmi inayotambulika na serikali kwa madereva kuwa na mikataba, posho, medical insurances, leave kama waajiriwa wengine...

Jeshi la polisi liajili sasa vehicle inspectors well qualified na wawe trained kulingana na mahitaji...na hawa wawe wanafanya road patrol kwa ajili ya random checks kwenye mabus na malori hasa brake sytems, tyres, power trains, engines nk.....hizi ziwe zinafanyika barabarani hasa wakati wa kula mnavamia mnasample gari kadhaa, bus stands kubwa na wakati mwingine kuyaita baadhi ya mabus na malori kwenye Inspecton centers..

Makampuni ya malori na mabus yaanze sasa kuajili well qualified engineers wenye elimu, exposure na uzoefu unaohitajika kwa ajili ya management ya haya magari... Serikali iyakague haya makampuni kwenye ajira zake na watu inaowaajiri pamoja na mishahara kwa watu wao..

Tanroads waanze sasa kufanya road patrol za mara kwa mara pamoja na kuwa temporary road signs incase kuna fault mahala barabarani imetokea, kuwe na quick repair ya pits, mawimbi nk...wawe na link na jeshi la polisi pamoja na watumiaji wa barabara hasa mabus na malori kuwe na online daily breafing kwa mabus yote yanayokuwa barabarani kwa kila eneo kupata daily roads updates...

BILA KUFANYA HAYO TUTAKUWA KILA SIKU TUNAOKOTA MAITI , KUHARIBU BARABARA, KUHARIBU MALI, NA KUENDELEA KUKUZA JAMII MASIKINI.... tuache upumbavu na kuishi kama zama za mawe..
Umeongea points tupu, matajiri wakisoma hii roho na nafsi zao zitawasuta.
 
Back
Top Bottom