MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,238
- 50,411
Shemeji wangu (bwana wa dadangu) alipatwa na ajali, na sasa yupo amelazwa hospitalini hapa kwetu Nairobi na kuwa kama zezeta fulani.
Anajinyea na kudondokwa na udenda, lakini muda wote mke wake yupo anamshughulikia. Anamlisha, kumnywesha na kumuosha.
Nimejifunza mengi sana kutokana na haya majanga ya shemeji. Wazazi wake ni marehemu, sasa ndugu zake na binamu wao wanampa pole na kujiendea kwenye shughuli zao. Amebaki tu na mkewe ambaye yuko radhi kufanya yote.
Kwa kweli tuwapende hawa wake zetu, tuwaheshimu na kuwatunza maana hujui wala kufahamu iko siku utamtegemea kwa kila kitu.
Hata kama lazima uwe na mchepuko, hakikisha mke wako upo naye sawa na unamtunza kabisa.

Last edited by a moderator: