Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nimesoma habari kuwa ajali imetokea huko Dodoma usiku wa Jumapili 29 December wakati lori lenye namba T364 AZZ lilipokuwa likijaribu kukwepa shimo kubwa barabarani liliigonga Coaster yenye namba T846AYU na watu sita kufa hapo hapo. KUna majeruhi wako hospitali wengine ICU.
Kutokana na tukio hili polisi wanamshikilia dereva wa lori.
Acha tuseme ukweli humu JF. Ajali hii imesababishwa na nani hasa? Je si uzembe wa Tanroads katika kufukia mashimo makubwa barabara kuu na kuyaacha kwa muda mrefu? Hivi ndio tuseme Tanroads, hata kama hawana fedha za kuziba mashimo kwa lami, wameshindwa hata kuyafukia kwa mchanga ili kuepusha ajali za uzembe wa Tanroads kama huu?
Je, huyu meneja wa Tanroads wa Dodoma, ni mara ngapi anatuma vikosi kukagua barabara katika mkoa wake na kuhakikisha hazina mashimo yanayoweza kusababisha ajali? Je Mfugale ameweka huu utaratibu kwa Mameneja wote wa Tanroads mikoani? Mimi ni dereva, na nimewaki kuepuka kifo kwa kuingia porini baada ya basi kuingia upande wangu wakati dereva akikwepa shimo kubwa barabarani. Dereva wa basi hata aliniomba msamaha na kusema hakujua kuna shimo kubwa hiyo sehemu. Na mara kadhaa nimeingia mashimo makubwa ya ghafla barabarani.
Labda swali kubwa kuliko yote ni kwamba kwa kila lita ya dizeli au petroli tunayonunua, kuna fungu linaloenda Tanroads kwa ajili ya kurekebisha barabara. Ndio tuseme fedha hizo hazitoshi hata kufukia mashimo makubwa barabarani kwa kokoto na mchanga kama hawawezi kuziba kwa lami?
Acha tumsifie Mfugale kwa kujenga flyover na kuzipa jina lake, lakini kwa hili la mashimo makubwa yanayoachwa kwa muda mrefu katika barabara zilizo nchini ya Tanroads hawezi kukwepa lawama. Ndio maana nasema wazi kuwa Polisi wanamuonea dereva wa lori katika ajali hii. Waliosababisha hivi vifo vya watu sita na vingine vingi pamoja na uhalibifu wa mali vinavyosababishwa na mashimo makubwa ya ghafla barabarani ni Tanroads.
Ninachotaka kuona ni kimoja tu - Magufuli atoe amri kwa Mfugale kwamba kuanzia sasa sitaki kusikia ajali imetokea kwenye barabara kuu za lami za TANROADS na chanzo eti kulikuwa na gari ikikwepa shimo dereva aliloona ghafla katikati ya barabara.
Je tumesahau ile ajali ya Mafinga iliyoua watu zaidi ya 40 palepale ilikuwa tu ni suala la uzembe kama huu ambapo upande mmoja wa barabara ulikuwa haupitiki na basi (Majinja) ikagongana na lori katika kukwepa upande wa barabara usiopitika?
Reference: Sita wafariki dunia kwa kuparamiwa na lori

- Fanya ukaguzi wa kila wakati wa barabara kuu zote za lami na kuhakikisha eidha mashimo yamefukiwa permanently au kwa hatua za muda
- Shimo lolote lililofukiwa kwa hatua za muda sehemu hiyo iwekwe alama za tahadhali kwa madereva kuwaonya juu ya uwepo wa shimo kubwa barabarani. Kwa hiyo wakaguzi watembee na alama za onyo kuweka barabarani
- KIla mvua kubwa ikinyesha TANROADS wapite kufanya ukaguzi barabarani kuhakikisha hakuna vifusi vilivyuporomokea barabarani. KUna ajali ilitokea mikumi kutokana na hili
- KIla Mkoa wa TANROADS uwe na kikosi cha kazi cha kurekebisha barabara kwa muda na kiwe on call masaa 24 kwa siku katika siku saba za juma
- TANROADS wawe na call centre ya road emergency na watoe namba za simu za emergency au watumie 112 ili madereva wanapoona hali mbaya barabarani wawapigie na watatue hilo tatizo mara moja. Namba hizi zitangazwe kikamili pamoja na kuwekwa kwenye stika za insurance ili watu wazione na kuzijua