Akilinjema
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 11,433
- 11,747
Ni shida sana, kuna barabara ya lami imejengwa goba-makongo imejazwa matuta hadi unashangaa, kila mita 100 unaruka tuta. Yaani unajenga barabara nzuri ya lami unaishia kuiharibu na matuta. Unaishia kusababisha usumbufu kwa madereva na kuwaingiza gharama za matengenezo ya shock up na gharama za mafuta. maana utaendesha hapa na hapa unapunguza mwendo kuruka tuta
Wabongo wengi wanatabia ya kuendesha magari kwa mwendo kasi kinyume na matakwa ya kisheria!
Maeneo hayo ni makazi ya watu kwanini muendeshe magari kwa mwendo kasi?
Halafu ukiona sehemu imewekwa mafuta mengi mara nyingi kunakuwa na tukio au matukio ya historia ya ajali mbaya, kwa hiyo wanaweka matuta kama tahadhari watu wapunguze mwendo!
Sheria ya usalama barabarani iko wazi mwendo wa maeneo ambayo ni makazi ya watu, mijini, n.k
Kwa hiyo uwepo wa hayo matuta ni sahihi kabisa!
Sent using Jamii Forums mobile app