Mkuu inawezekana hakuna sheria ya kuwashutaki Tanroads kama msimamizi wa hiyo barabara though anatakiwa kuwa responsible hata bila mahakama.Nimesoma habari kuwa ajali imetokea huko Dodoma usiku wa Jumapili 29 December wakati lori lenye namba T364 AZZ lilipokuwa likijaribu kukwepa shimo kubwa barabarani liliigonga Coaster yenye namba T846AYU na watu sita kufa hapo hapo. KUna majeruhi wako hospitali wengine ICU.
Kutokana na tukio hili polisi wanamshikilia dereva wa lori.
Acha tuseme ukweli humu JF. Ajali hii imesababishwa na nani hasa? Je si uzembe wa Tanroads katika kufukia mashimo makubwa barabara kuu na kuyaacha kwa muda mrefu? Hivi ndio tuseme Tanroads, hata kama hawana fedha za kuziba mashimo kwa lami, wameshindwa hata kuyafukia kwa mchanga ili kuepusha ajali za uzembe wa Tanroads kama huu?
Je, huyu meneja wa Tanroads wa Dodoma, ni mara ngapi anatuma vikosi kukagua barabara katika mkoa wake na kuhakikisha hazina mashimo yanayoweza kusababisha ajali? Je Mfugale ameweka huu utaratibu kwa Mameneja wote wa Tanroads mikoani? Mimi ni dereva, na nimewaki kuepuka kifo kwa kuingia porini baada ya basi kuingia upande wangu wakati dereva akikwepa shimo kubwa barabarani. Dereva wa basi hata aliniomba msamaha na kusema hakujua kuna shimo kubwa hiyo sehemu. Na mara kadhaa nimeingia mashimo makubwa ya ghafla barabarani.
Labda swali kubwa kuliko yote ni kwamba kwa kila lita ya dizeli au petroli tunayonunua, kuna fungu linaloenda Tanroads kwa ajili ya kurekebisha barabara. Ndio tuseme fedha hizo hazitoshi hata kufukia mashimo makubwa barabarani kwa kokoto na mchanga kama hawawezi kuziba kwa lami?
Acha tumsifie Mfugale kwa kujenga flyover na kuzipa jina lake, lakini kwa hili la mashimo makubwa yanayoachwa kwa muda mrefu katika barabara zilizo nchini ya Tanroads hawezi kukwepa lawama. Ndio maana nasema wazi kuwa Polisi wanamuonea dereva wa lori katika ajali hii. Waliosababisha hivi vifo vya watu sita na vingine vingi pamoja na uhalibifu wa mali vinavyosababishwa na mashimo makubwa ya ghafla barabarani ni Tanroads.
Reference: Sita wafariki dunia kwa kuparamiwa na lori
View attachment 1308620
Inawezekana sheria ya manunuzi inawabana Tanroads ku act immediately kwenye issues za minor repairs kama hizo. Kunauwezekana mkubwa Tanroads Dodoma wako kwenye process za ku attend hiyo dharura kwa kutumia sheria ya manunuzi ambayo hairuhusu ku process na kuanza kazi within hours. Kama sheria ya manunuzi ni kikwazo bora iwe amended ili kupunguza ama kumaliza kabisa madhara kama hayo.
Tanroads hawakwepi lawama kwani walitakiwa waweke alama za tahadhari kuanzia 100m kabla ya eneo usika. Wabgeliweka pamoja na alama zingine hata hata bumps za mchanga ili kulazimisha madereva wazembe wapunguze mwendo na hatimae kuepusha ajali kama hizo
Sent using Jamii Forums mobile app