Ajali Dodoma: Basi la Geita Express limegongana uso kwa uso na Fuso, watu wanne wathibitka kufariki

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Watu kadhaa wanahofiwa wamefariki dunia baada ya kutokea ajali iliyohusisha basi lijulikanalo kwa Jina la Geita Express kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 134 DXR katika eneo la Chinangali II Mkoani Dodoma.

Habari zaidi zinafuata.



AJALI YA BASI LA GEITA EXPRESS YAUA WATU WANNE

Watu wa nne wamefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa katika ajali ya basi la GEITA EXPRESS namba T 640 DLE linalofanya safari zake kutokea Dar es Salaam kwenda Geita baada ya kukongana na gari namba T 134 DXR Fuso katika kijiji cha Manchali wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Onesmo Lyanga akiwa eneo la tukio amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 10:30 Jioni na ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa gari aina ya fuso kujaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari nakusababisha ajali hiyo.

Majeruhi katika ajali hiyo wamefikishwa katika hospitali ya Uhuru wilaya ya Chamwino na wanaendelea kupatiwa matibabu, huku mmoja wa mashuhuda akitoa ushuhuda juu ya ajali hiyo.
 
Back
Top Bottom