AJALI: Daladala lagongana na Lori la kubebea Ng'ombe

kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
4,131
6,109
Nimepata taarifa kuwa kuna ajali kubwa imetokea ikihusisha daladala aina ya DCM na Lori la kubebea Ng'ombe, inakadiriwa kuna vifo na majeruhi wengi.

Nimeshindwa kufika eneo la tukio kutokana njia kufungwa na foleni kuwa kubwa.

Barabara ya kutoka Buguruni na kwenda Buguruni zote zinefungwa.

Mliopo eneo la tukio mtupe habari kamili.

===========
Picha Eneo la Tukio
1457498898217.jpg


b8136221e5455ea5f55b26508fd261ad.jpg


ImageUploadedByJamiiForums1457499001.622864.jpg
 
kama upo karibu na maeneo hayo harakisha uwahi eneo la tukio utoe msaada kwa majeruhi...
mkuu nipo kwenye daladala naelekea ubungo.dereva imemlazimu kupitia Rozana mpaka boma....may be kama tunaweza kuwahi kazini.
 
kama unatoka ubungo change barabara kabisa,nimepita ajali ni mbaya sana inawezekana masa mawili mbele barabara itafunguliwa,nimeshindwa kupiga picha polisi wapo na utaratibu wa kuweka mambo sawa unaendelea ,ukiangalia hayo magar hatar tupu
 
Duuu siku nyingine mbaya watu wameamka salama na kwenda mishemishe lakini hawakufanikiwa kufika na hawatarudi majumbani mwao tena...Mungu awarehemu marehemu wote na awasaidie majeruhi
Mkuu mshana Jr hata sisi tuliobaki tuendelee kusali sana...hakuna ajuae sec moja ya maisha yake.hao wangejua wangekubali kupoteza kazi zao na hata kulala njaa leo kulikwepa hilo janga but hakuna aliejua.
 
Yasemekana DEREVA wa lorry Mzima,kwenye DCM Yasemekana kulikua na watu kama 12 wote wamepoteza maisha Mtoto mchanga Ndio kanusurika
 
naombeni picha ya tukio,hiyo ajali imeondoka na mjomba angu alikuwa kwenye lorry jamani,ni mwili itabidi usafirishwe kwenda dodoma kwa mazishi
 
Back
Top Bottom