Ajali: Basi la Kampuni ya BM Coach lapinduka wakati likikwepa Kichwa cha Treni (kiberenge) maeneo Chekelei

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
Basi la Kampuni ya BM Coach limepata ajali ya kupinduka leo majira ya Alasiri Machi 4, 2019 wakati likijaribu kukwepa Kichwa cha Treni (Kiberenge) maeneo ya Chekelei wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akielezea kuwa dereva wa Basi la BM Coach, akitoka Arusha kuelekea Morogogo alishindwa kusimama katika kivuko cha Treni eneo la Chekelei Mombo, barabara kuu ya Segera/Same.

Ameongeza kuwa; wakati kichwa cha Treni kikikaribia eneo hilo na ndipo basi hilo likagongwa na kulala ubavu huku kichwa hicho cha Garimoshi kikiendelea na safari bila kusimama.

Hakuna taarifa ya vifo kwa sasa isipokuwa abiria kadhaa wamejeruhiwa akiwemo dereva wa BM Coach ambaye ameumia sana. Amesema kamanda wa polisi mkoa wa Tanga.
IMG_20190304_164403_531.jpeg
IMG_20190304_165231_413.jpeg
IMG_20190304_164253_119.jpeg
 
Poleni wote mliofikwa na Adha hiyo.

Kwenye hayo mapishano ya Reli, hakuna watu wanaocontrol magari(kusimamisha magari) pindi treni inapopita?

Au huo mtindo wa kufunga barabara kwa muda ili Treni ipite upo mijini tu?
Makutano ya njia za gar na tren huwa pameandikwa stop.

Kwahiyo ukifika hapo kama una gar yakupasa usitop then utazame pande zote kama hakuna kiberenge bas unaweza endelea na safari zako

Ni hayo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni wote mliofikwa na Adha hiyo.

Kwenye hayo mapishano ya Reli, hakuna watu wanaocontrol magari(kusimamisha magari) pindi treni inapopita?

Au huo mtindo wa kufunga barabara kwa muda ili Treni ipite upo mijini tu?
Huko kuna tahadhari ya mchoro (alama)tu, sasa usipopunguza mwendo na kuchukua tahadhari, litakalotokea ni juu yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni wote mliofikwa na Adha hiyo.

Kwenye hayo mapishano ya Reli, hakuna watu wanaocontrol magari(kusimamisha magari) pindi treni inapopita?

Au huo mtindo wa kufunga barabara kwa muda ili Treni ipite upo mijini tu?
Sehemu yeyote yenye kivuko cha reli unapaswa kupita kwa tahadhari .Nchi nyingine unasimama kabisa kuhakikisha usalama upo kabla ya kuvuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom