Ajali: Basi la Hood laua mmoja na kujeruhi 27

mge

JF-Expert Member
Dec 19, 2013
558
179
Mtu 1 amefariki na wengine 27 wamejeruhiwa kufuatia ajali ya basi la Hood lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Arusha kupinduka eneo la Melela Mlandizi barabara ya Morogoro Iringa kufuatia dereva kushindwa kulimudu wakati anakata kona. Source: RADIO1 STEREO
 
Mmh Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu! Majeruhi wapate nafuu.

Ila hizi gari za Mbeya Arusha huwa zinakimbia sana.Roho mkononi!
 
Umechanganya Melela iko Moro na mlandizi iko Pwani. Ni maeneo yakl tofauti. Sasa wapi mkuu?
 
Mtu 1 amefariki na wengine 27 wamejeruhiwa kufuatia ajali ya basi la Hood lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Arusha kupinduka eneo la Melela Mlandizi barabara ya Morogoro Iringa kufuatia dereva kushindwa kulimudu wakati anakata kona. Source: RADIO1 STEREO
Hood kaanza tena kuua watu? Mabasi yenyewe hayana insurance. Poleni majeruhi, mungu awaponye mapema
 
Umechanganya Melela iko Moro na mlandizi iko Pwani. Ni maeneo yakl tofauti. Sasa wapi mkuu?

No. Wewe ndp unachemka. Melela ziko km 3. Kuna Melela Kololo, Melela Mlandizi na Melela nzuri. Zote zipo Moro, karibu na Doma.
 
Ujingaaaa mtupuuu

Hujalazimishwa kuandika. Huu hapa chini ni Ujinga? kuwa mstaarabu watu wameumia na mwingine kapoteza maisha.
6836916.jpg

9062411.jpg
 
Hood kaanza tena kuua watu? Mabasi yenyewe hayana insurance. Poleni majeruhi, mungu awaponye mapema

Insurance gani unayoizungumzia mkuu,third party au comprehensive insurance?,na bima kama third party ni lazima kisheria,inamaana mabas haya yanavunja sheria mchana kweupe na yanaachwa tu na yanapakia roho za watu namna hii?Tuandikeni facts sio hearsaies jamani!
 
Jamaaani, mkono wa Mungu wa uponyaji upate kuwa juu ya majeruhi wapone haraka, na marehemu apumzike amani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom