Watu watano wamefariki dunia mkoani Arusha baada ya kuangukiwa na mti.Mti huo ulianguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Chanzo: ITV
Mungu azilaze roho za marehemu pema peponi.
-----
Wamepitishwa hapa kimandolu kama saa nne hivi. Baba ni mlinzi amerudi asubuhi hii hakuwa na hiyo taarifa. Kulikuwa na gari inamsubiri hapa kituoni Kimandolu, alivyoshuka kwenye daladala tu wakamchukua na kuelekea nae hospitali, watu wamemwombolezea sana kwa hiyo surprise.
----
Kutokana na mvua inayonyesha mfululizo Mkoani Arusha imeleta maafa makubwa katika familia ya mzee Jonathani Kalambiya{55} mkazi wa sokoni II katika kijiji cha kinyeresi wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya mti
mkubwa uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote watano.
Mkasa huo wa usikitisha ulitokea jana majira ya saa 7 usiku baada ya mti huo kung’olewa na maji uliangukia nyumba hiyo iliyokuwa jira na mti huo.
Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Charles Mkumbo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja watoto waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na watoto wawili wanafunzi wa mzee huyo ambaye ni mlinzi wa hospital ya ya Dr Mohamed ya Jijini Arusha.
Mkumbo aliwataka wanafunzi ambao ni watoto wa mzee Kalambwia ambaye siku ya tukio alikuwa kazini ni pamoja na Miliamu Jonathani(16) mwanafunzi wa kidatu cha pili wa shule ya sekondari ya Inaboishu.
Kamanda alimtaja mwanafunzi mwingine ni ambaye ni mtoto wa mzee huyo ni Grolia Jonathani(11) mwanafunzi wa shule ya msingi Kinyeresi iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Amesema watoto wengine wa mzee huyo ni pamoja na mtoto wa kwanza wa mzee huyo aliyetambuliwa kwa jina la Giliad Jonathani(31),Lazaro Lomnyaki
(26) na Best Jonathani(20).
Kamanda Mkumbo alisema kuwa mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake mana uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumla.
Alisema na kuitakia pole sana familia yam zee huyo kwani tukio hilo ni majonzi makubwa sana kwake kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na uvumilivu katika wakati huu mgumu kwake.
Kamanda Mkumbo ametoa wito na ushauri kwa wakazi wa Arusha kuchukuwa tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na kuacha kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.
Amesema kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga mengine hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukuwa tahadhali hiyo.