Ajabu ya kisiwa cha Mafia: Ujue mji usiojulikana uliozama baharini kisiwani Mafia

juma sal

Senior Member
Dec 18, 2011
156
88
Awali ya yote naomba nikuhakikishie ndugu msomaji kua hii sio hadithi ya kusadikika au tuseme ni stori ya kutunga, hii ni habari ya kweli tena ukweli mtupu unayoelezea habari USIOJULIKANA na iliyojificha kwa miaka mingi na kwa watu wengi sana.
Kutojulikana kwa jambo kunatokana na tatizo kubwa linalotokana kutoandikwa kwa historia ya kisiwa cha mafia kulinganisha na historia ya kisiwa jirani cha unguja au kilwa. Kisiwa cha mafia kina historia ndefu na yenye kuvutia zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita inayoelezea mafungamano ya kibiashara kati ya kisiwa hiki na nchi ya misri ya kale pamoja na miji mingine ya mashariki ya kati.
Kwa wenyeji wenzangu wa mafia nadhani wengi wanahisi nataka nizungumzie kisiwa cha chole, au mji wa kua ulikuapo katika kisiwa cha Juani, ama hata eneo la kisimani mafia lenye magofu yaliyoliwa na bahari, andishi hili linahusu mji ambao wengi hawaujui....naam tufuatane kuufahamu mji huu uliozama baharini.

Siku Fulani February 2013

Mtalii na mzamiaji (diver) Alan Sotton toka uingeleza akiwa na wenzake wakitumia helicopter toka Dar kwenda mafia kwa lengo la kutalii na kujaribu kutafuta eneo ilipojengwa ngome ya wareno kisiwani mafia wakati wa utawala wa wareno pwani ya Africa ya mashariki karne ya kumi na tano. Chopa akiwa juu katikati ya bahari karibu na kisiwa cha mafia kina Alan waliona jambo si la kawaida ndani ya bahari. Anasimulia Alan na ushahidi wa picha kua waliona kitu
kama eneo kubwa lililozunguushiwa ukuta mkubwa mithili ya uzio wa tofali kuzunguuka mji. Kwa haraka ungeweza kudhani labda ni miamba lakini sio kwa mafia kisiwa ambacho kijografia ni mchanga. Eneo hili linapatikana kaskazini magharibi mwa kisiwa cha mafia karibu na kijiji cha Chunguru ama tuseme Tumbuju ukiwa unaitafuta Jojo au Banja ni eneo la mavuvi ambapo wavuvi wenyeji wao hudhani ni mwamba tu. Baada ya kujaribu mara kadhaa kwa miaka mitatu mfululizo kulitafuta eneo hili kwa boti na kwa msaada wa mwenyeji wa mafia bwana athumani bakari, Alan hatimae March 21, 2016 akafanikiwa kufika eneo husika akiwa na mwenzie alietwa Jane Hannah na kuchukua picha na video kwa mara ya kwanza na kutuma katika mtandao wa seaunseen.
Kinachoonekana ni kuta za nyumba zilizobomoka pamoja msingi wake. Ukuta huo una urefu wa takribani kilometa 3.7 unaoanzia mashariki kwenda magharibi na upana wa kilometa moja uliokaa kusini/kaskazini. Tofali zake zikiwa na ukubwa tofauti nyingi zikiwa na ukubwa wa mita tano kwa mita tano na unene wa sentimita 40 (40cm). Tofali hizi zikiwa zimejengwa na malighafi tofauti lakini zinazooneka kiurahisi ni mawe aina ya sandstone na aina fulanifulani ya saruji. Kuta zikiwa zimejengwa kwa mtindo sawa na majengo ya kale yanayopatikana maeneo mengi ya pwani ya Tanzania. Ukubwa na mtindo wa ujenzi wa eneo hili bila ya shaka sio tu unatuambia kua ulikua mji bali ni mji wenye umuhimu wake.
Swali muhimu la kujiuliza ni mji gani huo? Nani na lini aliujenga? Na kwanini umezama?
Tunaendelea.......

The Periplus Maris Erythraei (‘Voyage around the Erythraean Sea’)

Haya ni maandishi ama tunaweza kusema kitabu kilichoandikwa na baharia-mfanyabiashara Mmisri aliekua anazungumza kigiriki asiefahamika jina lake katika nusu ya karne ya kwanza aliefanya safari kwa njia ya majahazi. Maandishi haya yanajikita zaidi kuelezea njia mbili za kibiashara kwa njia ya bahari moja ni east-west yaani toka misri kuelekea bara arabu na ashia kwa ujumla na yapili north-south yaani toka misri kuja pwani ya Africa mashariki mpaka Tanzania ya sasa. Mwandishi alikua anaelezea kuhusu urefu wa safari, njia ilivyo, misimu ya kusafiri, bidhaa za kwenda kuuza na kununua maeneo husika, watu na watawala pamoja na maeneo ya kutia nanga.
Sehemu ya kwanza mpaka ya kumi na nane ya kitabu hiki mwandishi anazungumzia njia ya north to south na mambo yake.
Kulingana na Periplus kusini mwa pwani ya afrika ya mashariki kulikua na soko kubwa la bidhaa mbalimbali zikiwepo meno ya ndovu na magamba ya Kobe, eneo hilo likiitwa Raphta likiwa karibu na kisiwa kilichoitwa Menouthesias. Mpaka hapa niandikapo wanahistoria wengi wanatofautiana kuhusu eneo hilo Raphta ilipokua, wapo wanasema Menouthesias itakua Zanzibar na Raphta ipo kati ya bagamoyo na Dar wakati wengine wakisema Raphta ipo kati ya Rufiji na na kilwa na Menouthesias ni Kisiwa cha Mafia. Lakini tangu miaka hiyo Raphta imekua kitendawili na ikitafutwa bila mafanikio na huwapelekea baadhi ya watafiti kudhani kua Raphta labda itakua imezama, katika ukanda wa pwani ya baharini ya Hindi katika maeneo ya mafia, kilwa na Rufiji. Kugundulika kwa magofu haya chini ya bahari wengi wanadhani kua 'RAPHTA IMEPATIKANA'

JE NI NGOME YA WARENO?
Miaka ya 1890 mpelelezi maarufu wa kijerumani ambao wengi wetu tulimsoma kuanzia darasa la tano aliefahamika kama Carl Peters alifika Mafia kukusanya taarifa zihusianazo na kisiwa hiki na moja ya jambo alilofanya ni kuchora ramani ya mafia na moja ya maelezo katika ramani ni uwepo wa NGOME ya wareno upande wa magharibi ya kisiwa cha mafia iliyobomelewa na kumezwa na bahari. Mbali na hayo ya Carl Peters, Marco Ramineri ambae ni mtafiti na mtaalamu wa makazi ya kale ya wareno alipata baadhi ya nyaraka za wareno za mwaka 1636 zinazoelezea uwepo wa kituo au ngome iliyokua ikilindwa na askari kumi na mbili. Licha ya maelezo yote hapo juu mpaka leo hii hakuna anaefamu wapi ngome hiyo ilikuwepo kisiwani mafia. Kwa kiasi Fulani wengine huhisi huu mji ni hiyo ngome ya wareno.

UMRI WA TUMBAWE WAONGEZA UTATA

Kwa kimombo matumbawe huitwa corals, Kwa wale wasioelewa tumbawe ni nini labda naweza kwa maneno machache naweza kusema ni viumbe hai venye maumbile tofauti tofauti vinavyoishi baharini na kua ni moja ya mazalia ya samaki. Sasa basi wakati Alan anafanya uchunguzi wa kina eneo hilo alikuta moja ya tumbawe aina ya porites corals limejishika katika moja ya ukuta lenye urefu wa mbili na nusu ( 2.5M) na kwa wastani aina hii ya tumbawe linakua kwa wastani milimita nne na nusu kwa mwaka (growth rate of 4.5mm per year)
Ukifanya hesabu hapo utagundua kua tumbawe hilo lina umri wa takribani miaka mia tano hamsini na tano (555). Hii ina maana gani?...Maana yake ni kua ukuta ule upo kwenye maji kwa zaidi ya miaka 555. Kwa maana hiyo majengo yale yalishazama kabla wareno kuja karne ya kumi na sita. Na hili linathibitishwa na ukweli kwamba kwa miaka elfu mbili iliyopita kina cha bahari kimeongezeka kwa mita nne tu kwa hiyo ni ngumu kuamini kua mji huu umejengwa karne ya kumi na sita au kumi na tano na eti labda umezama majini kwasababu bahari imeongezeka kina. Japo kuna ukweli unaothibisha kua matetemeko ya ardhi kama tsunami iliyoikumba dunia miaka kadhaa iliyopita imechangia kwa kiasi kufanya majengo haya yajichimbie zaidi lakini sio kufanya yafike kina ya mita tano wakati wa maji mafu.

Maoni ya profesa Felix Chami

Akielezea kitendawili hiki archeologist toka chuo kikuu cha Dar es salaam Profesa Chami anadhani kua huenda haya majengo yalijengwa na Wareno ambao nao walijenga juu ya magofu mengine waliyoyakuta eneo hilo.

HITIMISHO
Mpaka sasa hakuna alieweza kuthibitisha na kuelezea kwa kina na kitaalamu juu ya kitendawili. Na kwahakika itawachukua muda mrefu wasomi wetu kufikia hitimisho lisiloacha chembe ya shaka juu ya mji uliozama baharini. Mnakaribishwa kwa maoni na tafakuri
 
Attachments

  • List.docx
    15.9 KB · Views: 84
  • IMG_5226.jpg
    IMG_5226.jpg
    290.1 KB · Views: 286
  • IMG_5246.jpg
    IMG_5246.jpg
    336.3 KB · Views: 276
  • IMG_5296.jpg
    IMG_5296.jpg
    29.6 KB · Views: 231
  • IMG_5383.jpg
    IMG_5383.jpg
    277.5 KB · Views: 271
  • IMG_5395.jpg
    IMG_5395.jpg
    208.6 KB · Views: 276
  • IMG_5398-1.jpg
    IMG_5398-1.jpg
    15.3 KB · Views: 259
Hakuna mji uliozama,hizo coral kawaida tu kukumbana nazo ukiwa baharini.
Mafia, ipo,unguja,,kilwa, znz, bmoyo, na kuna kisiwa hapo pembeni ya pemba ni base ya wamarekani na uingereza wako majini daily kimazoezi.
Wangeshatoa hiyo habari zamani.
 
ahaaa Mafia..wenyewe hutamka kwa kuivuta..Mafiaaa..nashukuru kuwahi kufika hapo.
 
Huo mji utakuwa ni ni Raptha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom