Ajabu! Watanzania wanataka maendeleo ila hawataki kulipa, TRA kazeni hivyo hivyo

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,137
Kazi Iendelee..

TRA wanakusudia kuanza kukusanya kodi kutoka kwa wamiliki wa nyumba za kupanga za biashara na madalali ila cha ajabu watu wanataka maendeleo ya kila aina ila hawataki kulipa kodi.

Hao hao huwa wanasema TRA haikusanyi kodi, hao hao hawataki kudai risiti wakifanya manunuzi na hao hao ndio husema TRA haijabuni vyanzo vipya vya mapato na kupanua wigo wa mapato.

Sijui nani aliwaambia kuwa maendeleo ni jambo la lelemama na mnategemea pesa itoke wapi?

Hakuna maendeleo bila pesa na pesa zinatoka kwetu tofauti na hapo sijui tunategemea nini.

TRA msisikilize upuuzi, kazeni hivyo hivyo pesa ipatikane nchi ipate maendeleo. Huko kwingine hadi silaha za moto hutumika kudai Kodi.👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220823-170206.png
    Screenshot_20220823-170206.png
    61 KB · Views: 1
  • Screenshot_20220814-115922.png
    Screenshot_20220814-115922.png
    110.5 KB · Views: 1
  • 20220813_095348.jpg
    20220813_095348.jpg
    105.6 KB · Views: 1
sababu unalipwa buku 7 na CCM unahisi mambo yanaenda kizembe eeh. Siku ambayo serikali itaweka Transparency juu ya makusanyo na matumizi na kudhibiti upigaji ndio watu watalipa kodi kizalendo vinginevyo waendelee kupora hela kwa raia tu.
Kwa hiyo nikilipwa buku 7 harafu ccm wananilipia Kodi ya nyumba au?
 
Tatizo sio kkulipa kodi. Ata waweke kodi 50 % ila huduma zote za msingi mwananchi unapata mbona watu tutalipa bili kinyongo.
Ishu ni hela inaenda wapi
Sio mbovu ila haziridhishi na haziridhishi kwa sababu bajeti hazitoshelezi na sababu ni kutolipa Kodi ila mnadai huduma Bora, haiwezekani.
 
Kuna Mtanzania / Mtumiaji / Mnunuzi asiyelipa Kodi ?

Kila ukinunua kitu, ukinunua vocha n.k. unalipa Kodi..., Tatizo ni walamba asali na wale ambao wapo supposed kugawanya keki ni walafi na hawakidhi vigezo..., mlipaji hapati value for money....

Na hio mikopo tunayokopa kila siku unadhani ni nani atalipa kama sio vizazi vya watanzania ambao huenda hata hayo so called maendeleo wasiyaone
 
Hizo mlizokopa na mnazoendelea kukopa in trillions kwa miezi michache zimefanikisha mradi gani wa kuleta tija hadi sasa? Kila mkopo ni ujenzi wa madarasa ! Tozo ujenzi wa madarasa
Kiasi gani hizo? Unaelewa maana ya bajeti?

Ulivyo poyoyo,ukisikia serikali imeidhinishiwa mkopo kiasi fulani kwa miaka 2 au zaidi unadhani zinakuja zote on the spot?

hii Nchi ni kubwa ina mahitaji lukuki ila kwa kuwa mbakula bure huko Dam kwa wajomba zenu ndio maana mnaongea upumbavu.
 
Sio mbovu ila haziridhishi na haziridhishi kwa sababu bajeti hazitoshelezi na sababu ni kutolipa Kodi ila mnadai huduma Bora, haiwezekani.
Huwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja lazma uwe na kipaumbele. Serikali lazima itumie akili kama ambavyo raia anatumia akili kutafuta na kuweka spending pattern inayoeleweka. Lazma kuwe na vipaumbele.

Hela inayokusanywa inatosha sana kama itatumika ipasavyo.
 
Huwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja lazma uwe na kipaumbele. Serikali lazima itumie akili kama ambavyo raia anatumia akili kutafuta na kuweka spending pattern inayoeleweka. Lazma kuwe na vipaumbele.

Hela inayokusanywa inatosha sana kama itatumika ipasavyo.
Ndio maana kuna Vipaombele kama maji,afya,elimu, barabara na kilimo.
 
Back
Top Bottom