Ajabu: Serikali ina hisa 10% tu katika Mradi wa Kinyerezi III

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
HISA ZA KINYEREZI III (600 MW)

Taarifa tulizopewa ni kwamba TANESCO ina 10% ya hisa zote (?) na SHANGTAN 60%.

Ninahisi gharama za US $ 342M ni zile za kuanzia ujenzi wa 300 MW.

Je 30% ya hisa zilizobaki zitauzwa kwa mtindo gani? Uuzaji huo uwe wa wazi na Watanzania wapewe kipaumbele.

Tumechoshwa na mikataba ya siri ambayo kwa kawaida ni mibaya kwa uchumi wetu.

TANESCO na SHANGTAN wakaribishe Watanzania wanunue hisa zilizobaki (30%).
 
Halafu Magufuli on the same.day alipoenda kuzindua huo mtambo wa Kinyerezi alipiga marufuku private companies kufanya power generation kinyume na sheria inayoruhusu mambo hayo.

Basically serikali yake inasema anataka nchi iwe ya viwanda wakati haina capacity wala resources za kuzalisha umeme let alone kufanya transmission au distribution. Unawezaje kuwa na kiwanda huku huna umeme wala barabara au reli ya kusafirisha hizo bidhaa unazozalisha hiko viwandani?

Sasa analazimisha pension funds wa invest pesa za wachangiaji kwenye viwanda visivyo na umeme na sio infrastructure matokeo yake shirika moja la pension wameamua kutumia pesa za wachangiaji kujenga ma bwawa ya samaki kwenye nchi iliyozungukwa na bahari na maziwa.....!!!!

Huyo ndio Magu. Anataka viwanda na PPP lakini anapiga vita private sector. Basically anapingana na sera ya serikali/chama chake na bajeti ya waziri wake wa fedha.

But again tulimchagua wenyewe na kabakisha 9 yrs and 4 months
 
Hii ndio mikataba bunge ilipaswa kuijadili sio kushindana kufukuzana bungeni kuviziana kama fumanio! Hii nchi ina vituko sana! Serikali imeanza kulala usingizi tulisema utumbuaji majipu ni nguvu ya soda mkasema ikiwekwa gongo itakuwa nguvu mpya yetu macho movie na iendelee
 
Bunge lipi mkuu?
 
Hv huu mradi FEDHA ZILIKOPWA CHINA... na bado hawa SHANGTAN wana 60% ya mradi wa KINYEREZI III..?❌❌❌❌❌❌❌✂✂✂

Huu ndio uwizi sasa... Hii inauma sana sana, Gesi yetu, hawa wachina wamepewa na nani hiyo 60% ya KINYEREZI III...?

Mh. Rais Magufuli, tunakupenda sana... OKOA NCHI HII.. TUOKOE.. NA HIYO 60% utakuta kuna mkono mtanzania na mm nahisi kabisa JK lazima anajua nn kinaendelea hapa.. haiwezekani GESI iwe tayari wachina wana 60% ktk hiyo 600 MW.... no.. no... nooo...!!

Mh. Rais Magufuli, OKOA NCHI HII... PLZ
 
Hakika Mkuu! Kifua changu kinajaa hasira kila nikiona unyonyaji ndani ya sehemu nayostahili kunenepa. ila kuna watu wachache nchi hii ku-Maa Ninaa Zao hawajai hata kwenye kiganja wanatufanya wananchi 45m kuwa ombaomba tusiostahili, hakika naapa lazima ni GAIDI na adui namba moja wa hizi siri kali za kisenge
 
Sasa alikwenda kufunguaje mradi wa wageni tena wachina? Ni kwanini wachina hawakumwalika rais wao kuwafungulia new china country in africa kwani sisi tunawalisha watu wao kwa nguvu zetu? Yaani aliwasha magari yote yale kwenda kufungua mradi wa shs. 10/=kwa kila 100/=! Na mbwembwe zote zile za kumzodoa meya wa ukawa sijui diwani kwa 10/=? Nasema tena aitable mikataba yote mezani tujue kilichomo na waliohusika wcawepo ili natural justice itamalaki. Figisu yoyote isichekewe hata kama ni malaika alihusika aitwe na ajibu mradi huo uliokopewa fedha nyingi kapewa mchina.
 
Kwa bahati nzuri au mbaya wabunge majembe wote wameletewa figisu za kipuuzi ili baadae mambo yakiianza kutibuka serikali isichezeshwe mputa. Huu ni udu wanzi wa kiwango chake katika hi sirikali.
 
Ah ah ah ah viruses wa lumumba siwaoni humu, mbona gas imeshapanda ndege kitambo ipo China wanaifanyia test miaka 7
 
Kama mna kumbu kumbu Mzee Nyerere aliwahi kumshika mtu baada ya kusema serikali yote ya Tanzania hiko mfukoni kwake lakini lile neno lina maana hadi hii leo hivyo usishangae serikali kuwa na kiasi hiko cha hisa.

Mwanasiasa mmoja mchangamfu alisema tulieni tulieni kuna mengi kisha akachombeza na "achukuchaaa"
 
Mkwawe,
Punguza hasira mkuu, GAIDI ni theory walizojiwekea weredi wa chache wanaowatumia binadamu wanzao(vifaa vipofu/blind instruments) kutimiza malengo yao na ubinafsi wao, Usiingie huko. Nchi bado inakuhitaji,Tatizo nchi hii tunahitaji mambo makubwa lakn uwezo wa kudecode rasilimali zetu ili zitunufaishe Uko chini sana. Amua kuweka malengo ya kuwa Rais ili siku moja utimize kile unachozani ni sahihi au la Achana na siasa Badilisha eneo dogo ulilopo liwe mfano na chanzo cha furaha maishani mwako. Ukiumia sana unaweza kusahau kuwa wewe leo usipokuwepo utatuachia wajane,watoto yatima na ombaomba,wazazi wako wanaweza kufa kwa njaa kama wanakutegemea. Ukikataa kuwa mwanasiasa kubali kutawaliwa na hao usiowataka na waache wafanye wanavyojisikia.
 
Magufuli analifahamu hili? najua machungu yake yapo kwenye mambo kama haya...
 
Nilitabiri hizi hasira! Kuna mambo mengine ukiyasoma au kusikia unapata presha! Lakini tupunguze jazba tutafute njia. Wanasheria na wabunge mna nafasi yenu msizisaliti nafsi zenu na wananchi wenu! wanahabari tumieni kalamu zenu kuleta ukombozi
 
HISA ZA KINYEREZI III (600 MW)

Taarifa tulizopewa ni kwamba TANESCO ina 10% ya hisa zote (?) na SHANGTAN 60%.

Ninahisi gharama za US $ 342M ni zile za kuanzia ujenzi wa 300 MW.

Je 30% ya hisa zilizobaki zitauzwa kwa mtindo gani? Uuzaji huo uwe wa wazi na Watanzania wapewe kipaumbele.

Tumechoshwa na mikataba ya siri ambayo kwa kawaida ni mibaya kwa uchumi wetu.

TANESCO na SHANGTAN wakaribishe Watanzania wanunue hisa zilizobaki (30%).
Paka hapo ulipotupa hii habari sio siri tena. Thanks
 
Back
Top Bottom