Ajabu sana, Waziri anakiri watanzania ni masikini halafu bado anaweka tozo

Mufti kuku The Infinity

JF-Expert Member
Sep 21, 2019
2,464
3,576
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi ishu ambayo imekua gumzo nchini kuhusu masuala ya tozo kwenye miamala ya simu na benki ambapo hizi ni baadhi ya nukuu ya alichokisema.

“Kwanini mwaka huu tozo ziliendelea tena?, tumeendelea tena kwasababu tumeshafanya kwenye madarasa na vituo vya afya lakini kuna mambo ya msingi ambayo yana umuhimu wa kuchukuliwa hatua kwa haraka sana”

“Tunahitaji kuweka nguvu kubwa sana kwenye shughuli za uzalishaji, tatizo la ajira kwa Vijana ni kubwa mno, Watu wasio na kipato nchini ni wengi sana, kila wanapomaliza darasa la saba kuna Watoto laki mbili hawaendelei na kidato cha kwanza na kila wanapomaliza kidato cha nne kuna Watoto karibu laki tatu hawaendelei kidato cha tano, tumewahi kujiuliza wanaenda wapi na ‘future’ yao ipoje?”

“Tumeshajiuliza wale wanaohitimu na hawaingii Ofisini wanaenda wapi!?, hakuna Kijiji hata kimoja ambacho hakina Mhitimu ambaye hana kazi ndio maana Rais anasema tuweke nguvu kubwa kwenye shughuli za uzalishaji, ndio maana tumeweka pesa nyingi kwenye kilimo ili Vijana wengi watengeneze kipato…. hawa ambao hawana ajira”

“Mnyororo wa umasikini mkiubariki inakuwa unabaki hivyohivyo haundoki kwahiyo zaidi ya Trilioni 1 zimeenda kwenye kuongeza nguvu kwenye uzalishaji upande wa kilimo, uvuvi, Wamachinga” ——— amesema Waziri Nchemba,
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Top Bottom