Elections 2010 AJABU: Kikwete amepata kura nyingi kuliko Dr. Slaa kwenye Jimbo la Mh. Mbowe?

kura zinazotangazwa ni kati ya Msimamizi na Tume na sio za vituoni. Kwa hilo linawezekana!!
 
Ndiyo maana tunatakiwa kupata vielelezo vya kutosha, tunaamini si wote waliopewa jukumu la kuchakachua wanampenda JK wapo watakaofanya deliberately kupotosha ili aingie mtegoni mfano kushinda JK jimbo la hai ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.Hapo ndiyo tutapata pa kuanzia
 
Assuming JK kupata kura sawa na alizopata mbunge wa CCM katika majimbo yote yaliyochukuliwa na upinzani. Je hii ingebadilisha sura nzima ya matokeo ya uchaguzi na kufanya upinzani kuchukua nchi?
 
Hili si jimbo lile, ambalo pamoja na lile la Arusha Mjini, ambalo wakurugenzi wake wa uchaguzi, (yaani ma--Returning officers) walihamishwa ghafla kwani serikali ya CCM iliona walikuwa wanatenda haki? Madhumuni ya transfer hizo ni kuhakikisha CCM inayachukuwa majimbo hayo. Kwa Mbowe waliambulia kuchakachua kura za urais tu.
 
hao wachakachuajinao ni binadamu must watakosea tu au kubugi step hapondo watakapoiona dunia chungu,usicheze na figures smt zinaweza goma kuchakachulika
 
Ndiyo maana tunatakiwa kupata vielelezo vya kutosha, tunaamini si wote waliopewa jukumu la kuchakachua wanampenda JK wapo watakaofanya deliberately kupotosha ili aingie mtegoni mfano kushinda JK jimbo la hai ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.Hapo ndiyo tutapata pa kuanzia

Ofcourse hiki kiliwadanganya sana wengi kwa kampeni gani aliyofanya SLAA HAI amshinde JK HAI! wananchi wanajua dk asubiri, ila kwa sababu hana kazi kama mtikila ataandaa nyaraka aende Mahakamani
 
Haya yote yanafanywa kwa faida ya nani? Nchi? Watanzania? Hapana. Inabaki kuwa hasara kwa nchi na Wanzania wote. Tunazidi kupotea kimwelekeo kama Taifa
 
Kumbukeni haya majimbo yote yalikuwa ni ya CCM, kwa hiyo kuna wana CCM wengi sana kwenye hayo majimbo. kuweni wapole mmeshindwa mmeshindwa tu acheni visingizio wakuu wangu
 
Swahla sio kushindwa bali tunataka haki itendeke kila mahali na kama haki haipo basi na amani haitapatikana
 
Kwa tume hii hilo ni sawa huwa hawaoni aibu,ila mimi nawashauri chedema kukusanya data nchi nzima kutoka kwa mawakala wao na kuziweka hadharani,bila tume huru kazi tunayo,
 
Nchi ya matangazo ya data feki imeshapitwa na wakati. Kuna watu bado hawajagundua hilo....yale ya arusha, mwanza na kigoma ni uthibitisho tu wa nini watu wanataka.
 
kura zinazotangazwa ni kati ya Msimamizi na Tume na sio za vituoni. Kwa hilo linawezekana!!

Na muda si mrefu , JK na wanawe watona maana ya huu mchezo wanaoucheza kwa niaba ya mafisadi. Kumbuka mafisadi watakuwa salama, ila JK atatakiwa ajibu.
Bahati mbaya uchumi wa kujitegemea ameshindwa anategemea misaada. Na hao wahisani wameshaonya uchaguzi si huru. Watamnyima misaada, na hapo ndipo tutaanzia kuonja utamu wa maisha ya Ki Mugabe!
Hivi huyu ndiye JK aliyevamia Comorro kuondoa wachakachaji wa Demokrasia? Ndiye huyu aliye kuwa mbabe wa Mwai Kibaki kule Kenya?
Basi mwosha huoshwa, si muda naye watamsuruhisha tu. Ni swala la muda, and I do not pray for it to happen.....
 
Back
Top Bottom