Ajabu hili toka Katika Siasa za Afrika mpaka leo halijavunjwa! Huyu ndio baba wa Marais wote wa hovyo Afrika

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Aliyewahi kuwa rais wa Liberia Charles D.B King aliyezaliwa tarehe 12 March 1875 – na kufariki 4 September 1961) ndiye mpaka sasa anayeshikilia rekodi ya dunia katika vitabu vya kuweka kumbukumbu za maajabu vya Guinness Books of Records kwa kushinda kwa UChaguzi uliokuwa Batili ,wa Kihuni, Wizi wa kura ambao uliwah kupata kutokea toka ulimwengu huu kuumbwa. Huyu ndiye anashikilia rekodi ya kupigiwa kura na maruhani wengi zaidi kuliko wananchi wake.

Mwaka 1927 ulifanyika uchaguzi ambao watu waliokuwa wamejiandikisha kupiga kura nchini Liberia walikuwa 15,000. na yeye alipata ushindi wa kishindo hasa wa kura 234,000. lilikuwa ni tukio la kushangaza sana. kuwa katika uchaguzi ambao wapiga kura ni 15,000 waliojiandikisha. Mh Rais huyu alishinda kwa Kishindo kikubwa sana cha Kura 234,000 kuzidi idadi ya waliojiandikisha kwa zaidi ya asilimia 100.

Kuna wimbo unasema afrika kuna mambo. hayakuanza sasa toka kitambo. na huyu nadhani ndo amekuwa baba wa marais wanaoiba kura katika nchi za afrika.
 
hahahaa dah... nafikiri hadi wapinzani waliogopa kufuata sheria kudai haki yao....
 
Story yako ni kwa mujibu wa nani?
Ndio maana tunapewaga lile jina la wanyama kwa kutofikiri!!
 
hizo ni kura Ambazo kiongozi flani wa upande ule huwa anashinda.
 
Aliyewahi kuwa rais wa Liberia Charles D.B King aliyezaliwa tarehe 12 March 1875 – na kufariki 4 September 1961) ndiye mpaka sasa anayeshikilia rekodi ya dunia katika vitabu vya kuweka kumbukumbu za maajabu vya Guinness Books of Records kwa kushinda kwa UChaguzi uliokuwa Batili ,wa Kihuni, Wizi wa kura ambao uliwah kupata kutokea toka ulimwengu huu kuumbwa. Huyu ndiye anashikilia rekodi ya kupigiwa kura na maruhani wengi zaidi kuliko wananchi wake.

Mwaka 1927 ulifanyika uchaguzi ambao watu waliokuwa wamejiandikisha kupiga kura nchini Liberia walikuwa 15,000. na yeye alipata ushindi wa kishindo hasa wa kura 234,000. lilikuwa ni tukio la kushangaza sana. kuwa katika uchaguzi ambao wapiga kura ni 15,000 waliojiandikisha. Mh Rais huyu alishinda kwa Kishindo kikubwa sana cha Kura 234,000 kuzidi idadi ya waliojiandikisha kwa zaidi ya asilimia 100.

Kuna wimbo unasema afrika kuna mambo. hayakuanza sasa toka kitambo. na huyu nadhani ndo amekuwa baba wa marais wanaoiba kura katika nchi za afrika.
Mamamae
 
Back
Top Bottom