Aishi vipi na mkewe hali ya kuwa mkewe ni muathirika?

mkulubule

Member
Aug 3, 2016
70
45
Nilikua nikisikia tu kuwa unaweza ukashiriki kimapenzi na mtu aliyeathirika na usipate maambukizi, imemtokea kwa bro wangu, alioa miaka miwili iliyopita na kabla hawajafunga ndoa walipima wote wakiwa salama, na wamefanikiwa kupata mtoto ambae ana mwaka na miezi saba sasa, kipindi cha ujauzito uliongezewa damu katika harakati za kujifungua.

Mwanamke amekua hamuamini sana mumewe kwa kuwa ni mlevi sana, anarudi usiku wa mwanane mara nyingine mpaka asubuhi, mbaya zaidi kuna siku mkewe kamkuta na kondomu mfukoni mwa suruali, mwanamke alilia sana na kuongea sana na ushauri aliopewa na ndugu zake kuwa aende hospital kucheki afya yake kama yu mzima basi aombe talaka na aolewe na mwanaume mwingine.

Kwenda kupima akakuta ameathirika yeye na mwanae, mumewe hakuamini ikabidi waende wote hospitali kucheki mume hana, wameenda hospitali zaidi ya 4 mume hana, mume akapima tena baada ya muda still hakua nao. Je, kutokana na yale matusi aliyokua akiyatoa mwanamke kuwa mumewe kampa UKIMWI aishi nae vipi?
 
kwenda kupima akakuta ameathirika yeye na mwanae, mumewe hakuamini ikabidi waende wote hospital kuchek mume hana, wameenda hospital zaidi ya 4 mume hana, mume akapima tena baada ya muda still hakua nao.

je, kutokana na yale matusi aliyokua akiyatoa mwanamke kuwa mumewe kampa ukimwi aishi nae vipi? je

Hapo inahitajika elimu tu , mwambie aende ANGAZA watampa elimu ya kuishi na mtu
mwenye hiyo hali.
 
Hii uswazi kwetu tunaita MBWA KALA MBWA maana ni zaidi ya hatari
Mkuu hayaja kukuta, mbona kitaa tunao wengi sana
wanaoishi na ndugu au jamaa zao wa karibu wenye
maambukizi. yaani hujafa hujaumbika mkuu.
 
Aisee hii kitendawili ni ngumu sana.
Yaan pamoja na tabia za mume.. lakin mume hana, mwanamke ndio anao. Hiyo ni habar nyingine kabisa..
Sasa hapo ni mume kukubali au kukataa hali halis maana yeye ndio mzima.
 
kwakweli ni changamoto sn, ni kabinti cha miaka 23 ni msichana ambae anafanya ibada sn ,na analia sn anasema haja
Kwanza naomba kujua mtoto aliethirika ana umri gan kwa sasa?
huyo mtot ana mwaka na miezi 7 au nane hivi
 
Aisee hii kitendawili ni ngumu sana.
Yaan pamoja na tabia za mume.. lakin mume hana, mwanamke ndio anao. Hiyo ni habar nyingine kabisa..
Sasa hapo ni mume kukubali au kukataa hali halis maana yeye ndio mzima.
yaani hii ni bonge la changamoto
 
nilikua nikisikia tu kuwa unaweza ukashiriki kimapenzi na mtu aliyeathirika na usipate maambukizi,

Imemtokea kwa bro wangu, alioa miaka miwili iliyopita na kabla hawajafunga ndoa walipima wote wakiwa salama, na wamefanikiwa kupata mtotoambae ana mwaka na miezi saba sasa, kipindi cha ujauzito uliongezewa damu katika harakati za kujifungu.

mwanamke amekua hamuaimni sana mumewe kwa kuwa ni mlevi sana, anarudi usiku wa manane mara nyingine mpaka asubuhi., mbaya zaidi kuna siku mkewe kamkuta na kondom mfukoni mwa suruali, mwanamke alilia sana na kuongea sn na ushauri aliopewa na ndugu zake kuwa aende hospital kuchek afya yake kama yu mzima basi aombe talaka na aolewe na mwanaume mwingine.

kwenda kupima akakuta ameathirika yeye na mwanae, mumewe hakuamini ikabidi waende wote hospital kuchek mume hana, wameenda hospital zaidi ya 4 mume hana, mume akapima tena baada ya muda still hakua nao.

je, kutokana na yale matusi aliyokua akiyatoa mwanamke kuwa mumewe kampa ukimwi aishi nae vipi? je
Yawezekana aliupata ukimw kupitia kuongezewa damu kama utoaji Wa damu alikua window period yaan muda ambao vijidudu haviwez kuonekana bas akitoa damu hawawez kuonekana hao virus ,mungu ampiganie ktk changamoto hii kwan wanaume weng akijua MKE anahali hiyo humtelekeza Kabisa na haki ya ndoa kumnyima kabisa
 
mwaka na miezi 7 au 8
Kama mtoto ana mwaka na miezi 7 na bahati mbaya ni muathirika, nashauri.

1; Tatizo limeingia kwenye ndoa hakuna haja ya kutafuta mchawi, wanandoa wakae chini wakubaliane na jinsi ya kuishi kwa pamoja na kulea familia yao.

2; Waende kwenye kitengo cha wanaoishi na vvu kwenye hospitali zote za serikali hicho kitengo kipo, waende wote watatu, watapewa ushauri na kupimwa tena kwa umakini wote watatu, baba mama na mtoto.

3; Endapo majibu yatakuwa kama awali baba hana, basi watashauriwa jinsi ya kuishi maisha ya ndoa bila kuambukizana, ambapo baba atatakiwa kutumia kondom sahihi muda wote atakapojamiiana na mkewe na mke asichepuke kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi mapya pamoja na magonjwa mengine ya ngono.

4: Waathirika wataanzishiwa dozi mara moja.

Ni muhimu waende wote ili mtu wa afya awachunguze kwa makini,nasema hivo kwa sababi kipimo( sd bioline au unigold) majibu yake lazima usome ndani ya dakika 10 na zisizidi dakika 20, na kuna wakati mwingine mstari mwekundu unaonekana kwa mbali(very weak)

Kwa serikali; nashauri hii iwe funzo, mpango wa serikali kuthibiti maambukizi ya mama kwa mtoto(pmtct) usiishie pale mama anapojifungua, mama aliyezaa bila maambukizi bado afuatiliwe mpaka atakapoacha kumnyonyesha maziwa mtoto, Naswma haya kwa kuchukulia ya kuwa mama aliambukizwa alipoongezewa damu au mama alipata maambukizi baada ya kuujifungua.

Inasikitisha kwa kweli mtoto mdogo kama huyo kuanza kutumia arv, sababu ya uzembe wa madaktari au mfumo kuwa na mapungufu.

Kwa wakunga/watoa afya;
Ni uzembe au uuaji kukubali kumzalisha mama bila kujua hali yake ya kiafya, kuna uwezekano mama alikuwa muathirika wakati wa kujifungua na si kwa sababu ya kuongezewa damu.

Kwa wamama wajawazito
; epukeni kuongezewa damu wakati wa kujifungua kiuzembe, hakikisha una damu ya kutosha kabla hujajifungua,kula mboga za majani hasa matembele hata kama hayana latha

Poleni sana wanafamilia husika
 
Poleni sana wanafamilia husika[/QUOTE

Shukrani sn kwa ushauri mzuri ndugu yangu, TUTALIFANYIA KAZI.
 
kwa roho za kibinadamu sidhani kama kaka yako yeye atakuwa tayari kuishi na huyo mwanamke kwa sababu anaweza akayapindua hayo majibu kihisia kuwa yangekuwa ndiyo yake na kwa maneno yaliyokuwa yakisemwa means angekuwa ameshapigwa chini.

Ila laiti kama kungekuwa hakukuwa na hayo makelele kabla ya kupima basi jamaa angeishi na mke wake vizuri kabisa.
 
Back
Top Bottom