Aishi Manula sikia hili

Mpangumbe

JF-Expert Member
Jun 16, 2019
492
1,000
Salaam wakuu,

Binafsi ninaamini Aishi S Manula ndiye mlindalango bora wa kitanzania kwa sasa ila kuna jambo ananikera sana.

HAWEZI KUCHELEWESHA MUDA (nimemuona kwenye michezo mingi ikiwemo wa jana dhidi ya Benin) yani timu yake inaongoza bao moja na imeelemewa muda wote wanashambuliwa wao kisha anadaka mpira dk ya 75+ hata kulala halali wala kusingizia ameumia badala yake anainuka na kuanzisha mpira haraka unakera.

Ile kuchelewesha muda huwaudhi wachezaji wa timu pinzani na kusababisha kutoka mchezoni kwa namna fulani.

MANULA BADILIKA.
 
Hadrianus

JF-Expert Member
Feb 19, 2020
1,584
2,000
Mkuu mazingira ya kuchelewesha muda jana hayakuepo.

Hapakua na kugongana gongana na washambuliaji wa timu pinzani, afu wale ball boys walikua sharp sana kurudisha mipira uwanjani (goal kick).

Alijitahidi kutafuta mazingira ya kupoteza muda ila ikawa ngumu sana.

NB: Maoni yangu kulingana na nilivoshuhudia mchezo.
 
Mwadilifu Mdhulumiwa

JF-Expert Member
Jul 22, 2021
271
500
Mkuu tambua kuwa kila dakika ya mchezo imewekwa kwa ajili ya kucheza sio kufanya maigizo ya kujifaya umeumia! Binafsi sikualiani kabisa na mtindo huo!

Hivi hukuona kuwa kua kipidi cha dakika hizoizo Samatta alibaki kidogo atupatie goli la pili ? Sasa kujiagusha hovyo kama timu za Mwadui au Meya City huoi kama ni kujiaisha?

Tuwapongeze tu walipambana na kiume aisee!
 
Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
11,322
2,000
Mkuu mazingira ya kuchelewesha muda jana hayakuepo.

Hapakua na kugongana gongana na washambuliaji wa timu pinzani, afu wale ball boys walikua sharp sana kurudisha mipira uwanjani (goal kick).

Alijitahidi kutafuta mazingira ya kupoteza muda ila ikawa ngumu sana.

NB: Maoni yangu kulingana na nilivoshuhudia mchezo.
wale waokota mipira sijui walikuwa trained yani anamuwekea kabisa mpigaji mpira apige badala ya yule mpigaji kuuweka yeye
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,258
2,000
Salaam wakuu.

Binafsi ninaamini Aishi S Manula ndiye mlindalango bora wa kitanzania kwa sasa ila kuna jambo ananikera sana.

HAWEZI KUCHELEWESHA MUDA (nimemuona kwenye michezo mingi ikiwemo wa jana dhidi ya Benin) yani timu yake inaongoza bao moja na imeelemewa muda wote wanashambuliwa wao kisha anadaka mpira dk ya 75+ hata kulala halali wala kusingizia ameumia badala yake anainuka na kuanzisha mpira haraka unakera.

Ile kuchelewesha muda huwaudhi wachezaji wa timu pinzani na kusababisha kutoka mchezoni kwa namna fulani.

MANULA BADILIKA.
Kwa hili namtetea Manula, kijana wangu wa kutokea kule Chikago Mkamba morogoro. Kupoteza muda bila sababu ni hatari sana kwa timu yako.

Maana wachezaji wenzako watapunguza kasi ya kucheza na hivyo kuruhusu makosa, na kufungwa dakika za mwisho.
 
chenjichenji

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
1,675
2,000
Inawezekana pia ni maelekezo ya benchi la ufundi maana wao ndio waliokuwa uwanjani kwa hiyo ni rahisi zaidi kupeleka maelekezo kwa namna wanavyotaka acheze.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom