Aiseeh! Mke wa Mtu sumu

nelvine

JF-Expert Member
Nov 8, 2015
1,109
1,855
Habarini Wana Jamvi.

Nimeamini kweli Mke Wa Mtu ni sumu jamani, lilichonikuta mwenzenu basi nimekoma.

Picha Ilikuwa Hivi.

Week Iliyopita Nilipata Dili Furani Kijijini, Baada Ya Kufika Kule Katika Harakati Za Maisha Si Nikakutana Na Mlembo Wa Kijiji?
Mtu Mzima Nikaona Isiwe Taabu Mbona Mtoto Anajileta Tu Acha Niombe Mzigo, Hile Kamba Ya Kwanza, Ya Pili Pisi Ikasema Imenikubali Lakini Ye Kaolewa Japo Mumewe Kasafiri Kwa Mda Sasa.

Nkaona Isiwe Kesi Acha Nimwache, Lakini Binti Akagoma Akadai Nae Kanikubali Basi Tufanye Siri Yetu, Nikaona Isiwe Taabu Acha Nami Leo Nile Kuku Wa Kienyeji.
Basi Bwana, Tukapanga Miadi Mida Ya Kukutana, Kweli Pisi Ikaja Eneo La Tukio, Mzeee Nikaona Dah Mimi Ndiyo Mimi Acha Nifaidi Leo(Kumbe Nisilolijua Ni Kama Usiku Wa Giza).

Hile Tumeanza Show, Tukapiga Sana Hadi Mida Ya Usiku Mnene, Pisi Ikaomba Kuondoka Iende Kwao, Nikamsindikiza, Hile Narudi Om Kufika Kulala Tu, Nilianza Kuumwa Kichwa Na Tumbo Sanaaaaaa, Nikajitahidi Kuvumilia Lakini Wapi, Ikabidi Niamshe Wenyeji Nikawaambia Naumwa Sana, Nikapelekwa Zahanati, Tibiwa Sana Lakini Hamna Kitu, Kufikia Saa Tatu Asubuhi Nikawa Nmekufa Kimazingara(Nina Sikia Na Kuona Kila Kitu, Lakini Siwezi Kuamka Wala Kutingisha Chochote).

Nikaanza Kuona Watu Wanalia Wakidai Nimekufa, Hadi Yule Demu Nlolala Nae Usiku Alikua Analia Hadi Kuzimia, Taratibu Zingine Za Kuusafirisha Mwili Wangu Zikawa Zinaendelee, Wakati Huo Mi Nashuhudia Kila Kitu, Natamani Niwaambie Mimi Mzima Lakini Siwezi.

Wakati Wa Kunisafirisha Taratibu Zote Zilitimia Nikawekwa Kwenye Jeneza Kwa Ajiri Ya Kurudishwa Mjini, Bahati Ilioje Binti Niliyelala Nae Akamweleza Ukweli Mmoja Wa Wazee Wa Kile Kijiji, Ghafla Msiba Ukahairishwa Na Watu Kutawanyishwa, Na Mimi Kubebwa Na Kupelekwa Kwa Mtaalamu(Mganga Wa Jadi), Nikafanyiwa Dawa Masaa Karibia 6, Mungu Mkubwa Nikaamka Nikiwa Mzima Wa Afya.

Nikaulizwa Kuwa Je Nilitembea Na Yule Binti? Nikasema Ndiyo, Wakasema Una Bahati Sana Binti Alijisema Lasivyo Ungezikwa Mzima. Kumbe Kile Kijiji Ndiyo Tabia Yao Hiyo Wana Wafunga Wake Zao, Na Binti Hakujua Kuwa Mumewe Kamcheza.

Kumbe Mume Wa Binti Kamfunga Mkewe, Ukilala Nae Tu Unakufa Kimazingara, Unazikwa Ukiwa Mzima Utafia Kaburini, Aiseeee Nimekoma Siji Rudia Tena Mke Wa Mtu Mimi.

Nimekoma
 
Back
Top Bottom