Aisee!!, Saizi asubuhi asubuhi nimemaliza elfu saba(7,000)

Kuna sehemu moja hapa karibu na ushirika towers, kuna mgahawa wa wadada wa kichaga, wanaingia watumishi wa umma na maofisi ya pale jirani kunywa chai, lunch...

Pale ndio utajua watu wanakula mzee, supu ya samaki/sangara/sato au kuku, chapati mbili, mayai ya kukaanga, chai ya maziwa. Akimaliza anachukua juice nzito ya 2,000 na maji ya 1,000.
Ndio maana watumishi wa umma huwa wanasinzia sana maofisini, yani ukitaka huduma atakwambia mtandao upo chini kisa yeye kashashiba ndii anasinzia tu yaani
 
Kuna sehemu moja hapa karibu na ushirika towers, kuna mgahawa wa wadada wa kichaga, wanaingia watumishi wa umma na maofisi ya pale jirani kunywa chai, lunch...

Pale ndio utajua watu wanakula mzee, supu ya samaki/sangara/sato au kuku, chapati mbili, mayai ya kukaanga, chai ya maziwa. Akimaliza anachukua juice nzito ya 2,000 na maji ya 1,000.
Hawajui, mchemsho wa kuku ni sh 6,000, ongeza chapati 2 zilizochanganywa na mayai 2, juice ya buku na maji ya kubeba mkononi.
 
Huku kwetu kuna hadi supu ya jero....

Supu ya utumbo ya jero na chapati mbili 900

Ukitaka chai hadi mia tatu unakunywa, maandazi mawili ya miamia na chai ya mia.
300

Mchana ugali dagaa mixer maharagwe na mchicha au tembele kidogo 1000

Usiku sipendi kula sana...nakula muhindi wa kuchoma 300...usiniulize kuhusu maji ya kunywa...(900+300+1000+300)=2500

As income increases, expenses increase as well and vice versa...
 
Binafsi mpaka muda huu wa saa 14:06 nmetumia 1900/=
Nauli ya kufika kwenye mishe zangu 400/=
Juice ya miwa 500/=
Maziwa mtindi 1000/=
Sijanywa chai, nasubiri lunch
 
Daaa

Sijui ni anasa

Nimekula supu ya 3000/= bakuri kubwa kabisa, chapati 3(900/=)

Tamaa zikaja, nikaagiza juice ya matunda ya baridi hapa 1,000/=.,maji ya baridi 1,000/=

Nikanunua vocha ya 1000/=

Daa nimerudia matumizi yote sujaona nilipokosea kabisa, ila hela kubwa sanaa hio.

Bado mchana sijala, usiku bado ,bado kuna mpira jioni Man Utd inabidi nikaangalie (hapa inabidi niwe natumia mo energy ya barid nikiwa naangalia mpira hakuna namna )

Aisee inabidi leo nisimpigie demu wangu simu kabisa, asije nipiga mwiba mwingine!

Nilikuwa nimejiwekea kwa siku nisitumie zaidi ya 5000/= ndan ya uchumi huu wa magufuli(kazi za kuunga unga) naona mipango inafeli kabisa


Uzi tayar
Pale Pain killer inapozidisha maumivu badala ya kuyaondoa ndio shida inapoanzia.

Kuna kausemi wanakapenda watu wa pombe. DRINK RESPONSIBLY, NOT FOR SALE TO UNDER 18 AGE.

Na wewe sasa kuwa na EAT RESPONSIBLY au KULA KISTAARABU. HAIRUHUSIWI KUZIDISHA SHS 5,000 KWA SIKU.

Mkuu ni kanuni tu tena uliziweka wewe mwenyewe na kisha umezivunja wewe mwenyewe. Cha kufanya JISAMEHE, JIONYE NA JIPE KARIPIO LA KUTORUDIA TENA.😎
 
Daaa

Sijui ni anasa

Nimekula supu ya 3000/= bakuri kubwa kabisa, chapati 3(900/=)

Tamaa zikaja, nikaagiza juice ya matunda ya baridi hapa 1,000/= maji ya baridi 1,000/=

Nikanunua vocha ya 1000/=

Daa nimerudia matumizi yote sijaona nilipokosea kabisa, ila hela kubwa sanaa hio.

Bado mchana sijala, usiku bado, bado kuna mpira jioni Man Utd inabidi nikaangalie (hapa inabidi niwe natumia mo energy ya baridi nikiwa naangalia mpira hakuna namna)

Aisee inabidi leo nisimpigie demu wangu simu kabisa, asije nipiga mwiba mwingine!

Nilikuwa nimejiwekea kwa siku nisitumie zaidi ya 5000/= ndani ya uchumi huu wa Magufuli(kazi za kuunga unga) naona mipango inafeli kabisa


Uzi tayar
Daaah kwel uvhumi Wa Kati umekua mgum sana
 
Ungekua na mke hiyo hela mngekula kuanzia asubuhi mpaka usiku. Acha kula magengeni oa mke angenunua nusu kilo ya nyama ingekula supu mchana mpunga kitenesi usiku pilau la kizushi

Mabachela mnafeli sana
Dah.bado pale pale tu.....mkuu huko kuna mawigi..vipodozi...vikoba.....nk nk
 
Ina maana huna demu? Hayo mawigi, vocha, nguo ni gharama za kila mwanaume uwe umeoa au hujaoa
 

Ukiachana na umaskini ,technology pia ni kitu cha kuogopa sana,,asante mjumbe
 
Ngoja nikupe ujanja supu ya 1000, chapati 2 ni 500, juice ni 500, maji watakupa hapo hapo mgahawani yale ya kwenye tule tuglasi twa bati, mchana ugali dagaa na maharage na mboga mboga ni 1000, usiku wali 1500 kwa hiyo jumla 4,500/
Matunda muhimu mkuu "Eat more"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom