Aisee, kumiliki gari raha sana. Leo nimewapa lift watu 6 kwenye babywoka yangu!

Mlolongo

JF-Expert Member
Jul 4, 2019
3,269
5,890
Recently nimenunua gari ndogo (babywoka).
Sisemi gari gani lakin ni mojawapo kati ya haya matano (IST, VITZ, Passo, Honda Fit, Suzuki Swift)

Leo asubuhi sana kuna issue nilikua nawahi pale UDSM. Nilikua natokea Ubungo mataa, wakati nakunja pale kona ya njia panda ya Chuo (kuna kituo cha daladala na babaji nyingi wanapaki pale). Nikaona watu wengi wanapiga mkono kuomba msaada wa lift. Wengi wao walikua kinamama wanaofanya usafi na upishi katika cafeteria mbalimbali za UDSM.

Kutokana na kuwa wanafunzi wameanza likizo ndefu, daladala zinapita kwa kuotea sana pale. Kuna ile tunasema "I wish" kila mtu anakua nazo.
Mimi siku zote nimekua najisemea, "siku nikimiliki gari, nitakua nawapa lift kina mama, watoto wanafunzi wadogo wa primary na wazee hasa during rush hours au pakiwa na tabu ya usafiri". Basi mtu mzima nikaachia mafuta, nikawasha indicator ya kushoto, nikabonyeza breki pssssssssss... Nikasimama. Nikawaambia "pandeni niwasogeze".

Aiseee huwezi amini, kwenye kibebi woka changu waliingia wamama watano na askari wa usalama barabarani mmoja. Wamama wanne na yule askari walikaa nyuma. Halafu mama mmoja bonge kuliko wote alikaa mbele. Jumla watu sita, na mimi dereva tukawa saba. Aisee nilitamani nigeuke nyuma nione wale wamama wanne na yule askari walivokaa mpaka wakaenea kule nyuma 😂 😂 😂 .

Nikawasha indicator ya kulia (kuingia barabarani tena), nikakanyaga mafuta. Hapo nikawa nafikiria maneno ya Extrovert, joshua_ok na mng'ato wanasemaga eti "hizi babywoka hazina nguvu mlimani, tena ukiwa umepakiza watu wazima zikifika mlimani zinazima, au kutetemeka sijui nini bla bla". Nikasema leo ngoja nipime ukweli wa argument hiyo.

Kutoka pale njia panda kwenda utawala kuna kamlima kamechangamka halafu kana kona kona. Naonaga bajaji zikianza kupanda ule mlima zinaenda kama zinasindikiza bibi harusi. Lakin mie nikapanda huku nakanyaga kidogo kidogo gari inaenda vizuri tu. Hakuna cha gari kutetemeka, kuzimika wala kuishiwa nguvu. Nikafika pale Utawala yule askari akashuka akasema "asante kamanda". Wale wamama watano nikawaacha pale CONAS walivoshuka wakasema "asante sana baba, uwe unapita kila siku" wenzake wakacheka "heheheeee".

Nimejisikia faraja sana kuwapa watu msaada wa lift, hasa mida ile ya asubuhi "rush hours". Hatimae ndoto yangu imetimia kwa 50%. Magari mengi yalikua yanapita pale (tena ni wafanyakazi wa UDSM), kina mama wanapunga mkono kuomba lift hakuna anayesimama. Nasubiri shule zifunguliwe siku moja nipite kituoni niwabebe wanafunzi wa primary hata wawili tu niwasogeze hapo nitakua nimekamilisha "I wish" yangu kwa 100%.

Halafu kitu kingine nimegundua ukiwa unaendesha gari unapata heshima fulani hivi kutoka kwa watu barabarani. Bila kujali gari ni lako ama umeazima, bila kujali unaishi wapi au mfukoni una shingapi.

1599827370772.png
 
Recently nimenunua gari ndogo (babywoka).
Sisemi gari gani lakin ni mojawapo kati ya haya matano (IST, VITZ, Passo, Honda Fit, Suzuki Swift)

Leo asubuhi sana kuna issue nilikua nawahi pale UDSM. Nilikua natokea Ubungo mataa, wakati nakunja pale kona ya njia panda ya Chuo (kuna kituo cha daladala na babaji nyingi wanapaki pale). Nikaona watu wengi wanapiga mkono kuomba msaada wa lift. Wengi wao walikua kinamama wanaofanya usafi na upishi katika cafeteria mbalimbali za UDSM...
Gari ni sawa na ile sifa ya "Usomi" regardless umeishia level gani as long as umekanyaga chuo kikuu! Wewe ni msomi 🤣🤣🤣

Unapokea heshima nyingi sana ukiwa na gari. Tofauti na ambaye hana vijana wengi huwa wanaomba namba zangu tu.
 
Tahadhari: Sio kila unaempa lifti ni mtu mzuri, na usifikiri kuwa wengine hawatoi lifti kwakuwa tu wana roho mbaya,ni kwa sababu za kiusalama.

Umeshawahi kutafakari kuwa umemuona ni mwanafunzi au ni binti mzuri una mpa lift halafu ghafla akiwa ndani anageuka kuwa jini? Huo ni mfano tu iko mingi wengine wanaweza kuongezea....
 
Tahadhari:sio kila unaempa lifti ni mtu mzuri,na usifikiri kuwa wengine hawatoi lifti kwakuwa tu wana roho mbaya,ni kwa sababu za kiusalama.Umeshawahi kutafakari kuwa umemuona ni mwanafunzi au ni binti mzuri una mpa lift halafu ghafla akiwa ndani anageuko kuwa jini?huo ni mfano tu iko mingi wengine wanaweza kuongezea...

Nakupinga mzee. Wengi ni roho mbaya tu. Believe me! Mtoto wa primary darasa la tatu umpakize abadilike kuwa jini? Waafrika Waafrika
 
Nakupinga mzee. Wengi ni roho mbaya tu. Believe me! Mtoto wa primary darasa la tatu umpakize abadilike kuwa jini? Waafrika Waafrika
Huo ni mfano sio lazima iwe hivyo,hujawahi kusikia watu wametekwa magari kwa vitu kama hivyo?
 
Niliwai kupakiza watu wanne kwenye gari, baadae nafika home naona siti imechorwa chorwa na wamechukua triangle na matunda niliyoyanunua. Siku nyingine nimepakiza wanafunzi njian mmoja kapandisha shetani Kisha kafungua mlango na kujitupa nnje na kuumia mikono na miguu,

Niliwekwa ndani siku 2 maana wananchi walijua niliwateka na wazazi hawakuelewa kabisa mwisho baada ya kutoka ugomvi ukahamia kwa mke maana alijua yule dentist wa fom four Ni mchepuko. Tangu siku hiyo kupakia mtu Kwa gari labda niwe namjua au mtu mzima/mzee na matrafiki, wengine wanisamehe bure
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom