Aise, JK alishajua kuwa haya yatatokea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aise, JK alishajua kuwa haya yatatokea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kalamuzuvendi, Jan 11, 2011.

 1. k

  kalamuzuvendi Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Nanukuu sehemu hii ya Hotuba aliyotoa JK ya mwaka Mpya.

  Najua wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa ambavyo vimepanga mikakati ya kuendeleza malumbano yauchaguzi na kutaka Watanzania waishi kama vile nchi ipo kwenye kampeni za uchaguzi.Wamepanga wakati wote kutafuta jambo au hata kuzua jambo ili kuwachochea wananchi waichukie Serikali. Wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwamara. Kwao wao huo ndiyo mkakati wa kujijenga kisiasa ilikujiandalia ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

  Nawatanabaisha ndugu zangu myajue hayo ili msipoteze mudawenu muhimu wa kujiendeleza na kugeuzwa kuwa mbuzi wa kafara kwa ajili ya kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani. Kwa jinsi watu hao walivyokuwa wabinafsi na wasivyokuwa na huruma na wenzao, wako tayari kuchochea ghasia bila kujali madharayatakayo wakuta watu watakaoshiriki. Wao hasa wanachotaka nighasia kutokea na vyombo vya dola kuingilia ati waiambie jumuiyaya kimataifa jinsi Serikali yetu ilivyo katili. Nawasihi ndugu zangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hawa.Nawaomba, wakiwafuata wakumbusheni kuwa wao wanazo fursanyingi za kusema wayatakayo Bungeni na kwingineko, waachekuwatumia kama chambo au wahanga wa maslahi yao.

  Mwisho wa Kumnukuu.
   
 2. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo unahalalisha yaliyotokea Arusha?
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  So what?
   
 4. k

  kalamuzuvendi Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Hiyo nitafsiri yao wewe. Meseji ya JK ipo clear, alichosema JK ndicho exactly kilichotokea Arusha na sasa humu utaona watu wanasema serikali ya kikatili isiyojali watu wake...wengine wakijaribu kumwaga upupu katika jumuiya za kimataifa ili tu waonekane wameonewa.
   
 5. c

  cray Senior Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 172
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  BULL shit, what are trying telling us? He knew that people will not accept the way he is delivering, so he started by wornung people not to accept reality. Go to hell
   
 6. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  kwa upande mmoja, unaweza kuwa sahihi, kwamba JK amesema kitu. Ila alichosema kingekuwa na maana zaidi kama angeshughulikia matatizo yaliyopo kama Dowans na Tanesco etc etc. Au angekemea huo uchaguzi wa Arusha kabla. Otherwise ni pumba tu.


  HATA MIMI NAWEZA KUWANYIMA WATU CHAKULA, HALAFU NIKATABIRI KUWA LUNCH TIME IKIFIKA WATU WATAANZA KULIA NJAA NA WANAWEZA KUWA NA HASIRA.....

  wazungu wanasemaga........ DUH!
   
 7. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huo ulikuwa mpango wa Inteligensia ambayo walishawasiliana na JK ili ayaseme kabla hayajatokea. Hivyo JK alijua watu wataandamana na mpango serikali ni kufanya kile walichofanya Arusha. Ulikuwa mpango wao vile vile kwamba baadaye wasingizie kuwa Chadema wameleta vurugu.

  Kitu ambacho kinasumbua vichwa vya hao Intelijensia sasa hivi siyo namna ya kukabiliana na matukio yanayotokea bali ni kwa vipi wananchi wataaminishwa kuwa Dr. Slaa ni mtu anayeleta vurugu, ni mdini nk. na vile vile kuwa Chadema ni chama hatari.

  Walifanya jaribio la kuhadaa Watanzania wakati wa kifo cha Chacha Wangwe kuwa aliuawa na Chadema wakaishia kula matapishi yao. Hatudanganyiki
   
 8. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo wewe Mzuvendi sijui Mzulu unaona ni sawa kwa vile mkuu wa nchi alijua basi!!!!!!!!!! Waendelee kujichotea mafedha ya Dowans watu wanyamaze tuuu,na watoto wakose ada za vyou sawa tuuu, gharama za maisha zipande wewe sawa tuuu,unaishi nchi gani wewe????????????????? Labda uko USA (Mpe Mwanakijiji Adress yako!!) Watu kama nyinyi labda mnalipwa muandike kutetea uozo au kufikiri kwenu ni butu. Wewe endelea kutetea uchafu lakini siku moja yatakufika, utakumbuka watu wanadai nini????????????? Utakuwa umechelewa!!!!!!!!
   
 9. k

  kalamuzuvendi Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  sishangai mnavyoreply...si ndo kawaida yenu kutukana. Busara ni zero kwenu! Endeleen kutudhihirishia.

  More comments plzz.
   
 10. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Nadhani baba Riz1 alijistukia ama anajistukia. Anajua yapo mengi ya kumkosoa yenye ukweli. Alitumia nafasi ile kuelezea kuwa yeye ni muovu/sehemu ya maovu yanayotokea/yatakayotokea. Anadhani kukosoana ni kwenye kampeni za uchaguzi tu na baada ya hapo unaendeleza maovu.
  Kuna kila aja ya kuitia msukosuko serikali ili ijue kuwajibika ni kila wakati. Na pia afahamu maendeleo yanategemea serikali thabiti. Ni aibu kukosolewa na hata watoto wa shule ya msingi, nadhani hata 'nursery' wataanza kumnyima usingizi.
   
 11. MlongaHilo

  MlongaHilo Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Watanzania siyo wajinga wa kuburuzwa. Wanakubali kuandamana kwa sababu ndiyo njia ambayo sauti yao ya kuonyesha kutoridhishwa na uonevu unaofanywa. JK akitaka madhara yasitokee aache kuwakumbatia wanaoharibu taratibu na haki za wananchi.
  Ni kawaida kwa binadamu kuwa na levels za uvumilivu ambapo ukimbinya sana hufikia zero level of tolerance.

  TAKE CARE
   
 12. M

  Mapendoni Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli nimeamini na huku JF kuna watu ambao wameamua kuzipeleka akili zao likizo au wanaogopa kuzitumia kwa hofu kwamba zitaisha. Hivi kweli kwa madudu yanayofanywa na serikali unategemea watu wakae tu kimya? Walimu wanalilia maslahi yao wanaambiwa serikali haina fedha za kuwalipa, askari wenyewe waanaotumiwa na serikali ni wa kuonea huruma maana wanatumikishwa kufanya mauaji kwa ajili ya kutetea maslahi ya wengine bila kuona jinsi wanavyotaabika na familia zao kwenye umaskini. Ila malipo ya dowans yapo na wanajineemesha. Kama mtu ni msafi na unatenda yale unayopaswa kutenda sidhani km angeweweza kuyatabiri hayo. Anachokitaka ni kujaribu kuwatia hofu wananchi ili washoji uozo wa serikali. Pole sn ndg yangu maana na wewe ushakamatika
   
 13. semango

  semango JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  polisi kupiga raia risasi na kuwaua ni ukatili na uonevu na utabaki kua uonevu hata kama kichaa yeyote aliwahi kutabiri
   
 14. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  aaaagh!!!! nikisikia ishu yeyote ya Kikete NATAPIKA
   
 15. October

  October JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Unalipwa kiasi gani?
  Au amekuahidi kukuteua kuwa balozi nchi fulani?
  Tueleze ili tujue una maslahi gani kutetea wauaji wa watanzania!
   
 16. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mtindio wa ubongo unakusumbua. Ni kweli alisema na akaua watu sio ukatili huo? Kwa nini alisema kwa sababu aliingia madarakani kwa kuchakachua lazima atarajie upinzani na atayarishe nguvu za dola za ziada kubakia madarakani. Haiwazuii walioporwa haki yao kuidai hata kwa damu. Mbona wewe na yeye mnaweweseka mna jazba kwa nini kina wakera wakati kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi?
   
 17. k

  kalamuzuvendi Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Jazba unazo wewe na CDM, wewe ulitegemea nn polisi walipowataka mtawanyike then nyiny mkaanza kurusha mawe?
  By the way, JK hajaua mtu and he dd not offer anybody to killed in the riots, ila polisi wao walitumia moto kujitetea, uliona umati wa watu Arusha? Then umati ule ukupige mawe?? obviously moto ulipaswa kuwaka.
  Then kumbukeni hili litokea na ZNZ kwa CUF, moto uliwaka zaid ya AR, hamkulikemea hili..kulikoni ninyi watu? Mna agenda ipi?? tuelezen hapa, acheni porojo porojo na jazba...
   
 18. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hadi kufikia 2015 atakiona cha mtema kuni...ikulu sio pango la wanyang'anyi.
   
 19. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo inabidi polisi wakumbuke "akili mukichwa". Kama ilivyorukwa Richmond na Lowassa wake ndivyo watavyorukwa kwa kiherehere chao cha kuua wananchi wenzao kumfurahisha wanayedhani ni mwenzao mara mambo yakikorogeka.

  Kuhusu mauaji ya zenji 2001 sijui kama JF ilikuwa inafanya kazi. Watasema maveterani. Sie wengine hadi leo hatujawasamehe Mkapa na Mahita kwa hilo. Lakini chama chao kikisaidiwa na wa-TZ wengi hamnazo kinazidi kuwajengea jeuri. Tunashangaa tu CUF wameamua kulituliza suala hilo kama vile halikutokea bila hata kusisitiza angalau kuombwa radhi na (ikibidi) kulipwa fidia kwa wahanga au hata kuundwa TRC ili kuleta maridhiano ya kweli nchini kisha ndio Serikali ya umoja wa kitaifa ije.
   
 20. m

  mcheshi JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 769
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Hivi yeye mwenyewe ilchaguliwa na nani?mwizi tu.
   
Loading...