Airtel wapandisha gharama za kupiga simu?

Skype

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
7,266
1,631
Habari zenu wanajamvi. Jana nimepiga simu saa 2 usiku. Cha kushangaza ilikatwa tsh 300 kwa dakika 1. Kuthibitisha kua haikua bahati mbaya wakanitumia ujumbe usemao, "sasa piga simu kwa sh 2/sekunde kuanzia 12jion hadi 4 usiku".

Jamani nawasilisha, mwenye mchango zaidi karibu.
 
Habari zenu wanajamvi. Jana nimepiga simu saa 2 usiku. Cha kushangaza ilikatwa tsh 300 kwa dakika 1. Kuthibitisha kua haikua bahati mbaya wakanitumia ujumbe usemao, "sasa piga simu kwa sh 2/sekunde kuanzia 12jion hadi 4 usiku". Jamani nawasilisha, mwenye mchango zaidi karibu.

hama airtel
 
hahaha! Hamia tiGO bana. Gharama hazipandi kiivyo na hawanakili kutoka kwa wengine....
'SOTE NI NDUGU'
 
Habari zenu wanajamvi. Jana nimepiga simu saa 2 usiku. Cha kushangaza ilikatwa tsh 300 kwa dakika 1. Kuthibitisha kua haikua bahati mbaya wakanitumia ujumbe usemao, "sasa piga simu kwa sh 2/sekunde kuanzia 12jion hadi 4 usiku". Jamani nawasilisha, mwenye mchango zaidi karibu.

kama ni sh2 kwa sekunde, dakika moja ni sekunde 60, so itakuwa sh 120 kwa dakika. Ukiongeza vat 18% ya sh 120 ni sh 22 (approximately), kwahiyo jumla kamili kwa dakika ni sh 144 kwa dakika (approximately sh 150). Kwakuwa ulitumia sh 300 ina maana uliongea dakika 2 na sio dakika 1 kama ulivyoandika. Ubarikiwe!!
 
Ni kweli wakuu Airtel wamepandisha gharama zao even Tigo nao ss cha kushangaza mbona hawatangazi kwenye vyombo vya habari!!!nimeongea na customer care wameniambia ni mgao wa Umeme nchini na mtikisiko wa uchumi wa Dunia,nawakilisha
 
Nimegundua hawa jamaa ni majizi kama nini nimekaa na namba ya airtel tangu inaanza mpaka leo ninachoambulia ni kibano na majibu yasiyo maana kutoka cc. Yao hata ukiuliza kitu cha maana watakujibu utadhani ni mabaa maid. Kweli nadhani hii ni wiki yangu ya mwisho kuitumia no.yao najaribu kutulia nao lakini naona imekuwa kama ndoa ya kikristo MWEE NAHAMA!
 
Hamia koteeee!! TIGO usiende hao ni useless. Sehemu kama makumbusho, network ni hovyo! Tulia nao tu watarekebika. Vinginevyo utahama mpaka ukome ubishi!
 
hama airtel njoo tigo uone maisha yalivyo ndugu..
tena wanaweza kupandisha gharama za mawasiliano (airtel) muda wowote tena

njoo tigo tubanane ndugu
 
Hamia koteeee!! TIGO usiende hao ni useless. Sehemu kama makumbusho, network ni hovyo! Tulia nao tu watarekebika. Vinginevyo utahama mpaka ukome ubishi!

Wala hawana cha kujifunza na kubadilika hawa nimeshawavumilia sana najua makumbusho ndiyo maeneo yetu na pale Break Point sasa kama na wao ni vimeo nitakuwa napolea tu maana voda nao wamezidi uhuni hawana information zinazoeleweka wanakufanyizia halafu ukiwauliza ndiyo wanakwambia kuna mabadiliko wao nawatumia kwa mpesa tu baada ya hapo nazima line kabisa staki hata wanizoee.
 
Back
Top Bottom