Airtel wanazidi kutukamua

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,601
94,726
Leo nimejiunga na kifurushi cha sh 1900/-kwa mategemeo ya kupata dakika 40 kama nilivyozoea siku zote,nimeshangaa naambulia dakika 35 tu.Jamani mtandao huu unatupeleka wapi?
 
Umetumwa kubalance habari eeh?

Leo nimejiunga na kifurushi cha sh 1900/-kwa mategemeo ya kupata dakika 40 kama nilivyozoea siku zote,nimeshangaa naambulia dakika 35 tu.Jamani mtandao huu unatupeleka wapi?
Nimejaribu kununua kumbe nao wamepunguza kweli.... voda wamepunguza, tigo wamepunguza, hao nao wamepunguza. Kwa hiyo sisi tusio na comm allowance akili mkichwa.
 
Ni jambo la kusikitisha Sana,kwani badala ya angalau kubakia pale pale wanazidi kutukamua,na hatuna pa kukimbilia kwani hata Tcra wao wapo busy na kuuza ving'amuzi tu.
 
Mtandao gani ulio angalau nafuu tuwahame hawa wanyonyaji?
 
Mtandao gani ulio angalau nafuu tuwahame hawa wanyonyaji?

Nitakujibu kirahisi japo kimantiki na itabidi ukubaliane. Hakuna mtandao ulio nafuu, wote wanyonyaji wakiongozwa ama kusimamiwa na baba la wanyonyaji, serikali ya mipasho. Labda nikukumbushe kitu ambacho wengi tumesahau, kodi ya 1000 kwa mwezi kwa kila kadi ya simu. Sihitaji kukufumulia mengi zaidi nikakuongezea uchungu, wacha tulie ila ndiyo hivyo tunaumizwa sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom