Airtel wanawaibia wananchi, Bundle na Salio vinakombwa bila hiari ya Watu. Dowans? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Airtel wanawaibia wananchi, Bundle na Salio vinakombwa bila hiari ya Watu. Dowans?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Feb 4, 2011.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Hii inasikitisha sana, imekuwa ni mara nyingine tena pale ambapo watu wa airtel wanatumia uelewa wetu mdogo wa IT, kutuingiza kwenye hasara ambayo hatuitarajii. Wanachofanya wao ni kufanya kosa hilohilo mara kwa mara na kuomba msamaha. sijui kama TCRA wanalijua hili. Kwa wanaotumia modem za Zain, unakuwa umeweka bundle za kutosha lakini ghafla unaambiwa una sifuri.

  Ukiwapigia simu au kwenda customer care unaambiwa tatizo dogo limetokea utarudishiwa bundle zako. Kwa wale wenye line za Airtel unaweka mfano Tsh 2000/= unaongea muda kidigo kama dakika moja unaambiwa umebakiza sh 49/= ! hivi mambo gani haya. Mara ya kwanza walisomba fedha za watu na bundle wakasema samahani wakarudisha , na jana tena. Kwa hiyo wale bibi zetu na ndugu zetu walioko kijijini ambao hawana uwezo wa kufuatilia wala kupiga Customer care wameliwa na wanaliwa hivihivi kila mara.

  Anayetaka kuamini aende Airtel wamwambie wamekomba fedha kiasi gani za watanzania. Kama ni bahati mbaya kwa nini hawajitokezi hadharani kuomba radhi kila siku kosa lilelile, kama ni mpango wa kupata fedha fasta za kuwalipa Dowans tuambiwe. Watu tumeshindwa kutuma riport za kazi tunazozifanya sababu nyie mmelamba salio na bundle zetu. Wakubwa wetu wa kazi wanasema tuna viburi. Nikiachishwa kazi mjue mtautunza ukoo wetu wote nyie Aitel, mie ni mteja wenu ila mnaniboaaaa. Sasa nasema hivi rudisheni bundle zangu sasa hivi na salio mlilolamba kutoka kwa wananchi wengine, la sivyo...............

  Watanzania wengi hawajashtukia hii. Ukipiga huduma kwa mteja namba 100 unakaa mpaka dakika 24:03 umewekewa wimbo wala hawapokei maana wanajua wameshazua. Mie ushahidi nanao anayebisha nitatuma ushahidi wa walichonifanyia mara ya kwanza. Nasema kama tunalipishwa fedha za Dowans tuambiwe. Mie mkiona nimwaaribia biashara mkataka niwape namba yangu ili mnichakachue niko tayari lakini ukweli mie nausema, niwape numba, niwape ? Ole wenu niachishwe kazi maana sijatuma report hadi hivi sasa nilipokuja kutafuta internet cafe/ Boss kesha nuna aaahhh.
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Hivi ndivyo walivyonifanyia mara ya kwanza baada ya kufanya follow up


  Name:
  Number: Airtel-TZ
  Content:
  Dear Customer, We are working on your query. Your reference no. is 300215. We will contact you shortly.
  Time: 27/01/2011 11:46:16, NIKAZIDI KUWAMIND NA KUWAFUATILIA.

  BAADAE WAKATUMA HII

  Name:
  Number: AIRTEL
  Content:
  Mpendwa Mteja,Tunaomba radhi kwa kukatwa pesa zaidi ulipokuwa unatumia huduma yetu ya Intaneti.Tatizo limeshatatuliwa na utarejeshewa kiasi ulichotozwa zaidi
  Time: 28/01/2011 06:53:30

  NDO WAKAAMUA KUFANYA HIVI

  Name:
  Number: 15444
  Content:
  Asante kwa kutumia huduma za Airtel, Umetumia -523MB katika kifurushi chako cha 400MB .Umebakiwa na 923MB kifurushi chako kitamaliza muda wake 25-02-2011.
  Time: 29/01/2011 07:59:03
   
 3. M

  Mwera JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dawa nikuacha kutumia huduma yao ya internet,bora zantel wakojuu kwa internet nahawana wiziwizi kama huo,na wakizidi dawa yao nikutupa lain za airtel kwamkupuo,watakosa wateja watashika adabu,wahindi kila wanachoanzisha ktk tzania ni usanii mtupu,angali railway,sasa wataiua airtel aka zain.
   
Loading...