Airtel wana tatizo gani? Msaada wa kisheria

Ego is the Enemy

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
7,393
14,134
Habari wanajukwaaa.
Poleni kwa majukumu ya kuijenga Tanzania yetu mana ni Mali yetu site na sio kuwa ni ya MTU Fulani ama kikundi Fulani cha watu.
Nilenge shida kamili ni hivi:

Kuna mshkaji kwangu Wa karibu amelalamika juu ya hii kampuni na utoaji wao Wa huduma zao.
Ishu Iko ivi kuna Yale maduka wanayofungua Tanzania Nzima ila wanatumia wafanyabiashara binafsi kwa gharama zao. Hayo makubaliano yao ni franchise format. Wale watalaamu Wa biashara watanielewa. Ila cha kushangaza kuna eneo dogo wamewapa watu kama watano franchise mpaka anajiuliza kweli ndo makubaliano yalivyo ya franchise. Mana yeye ni Wa kupewa mktaba na kusaini bila ya kuyasoma kwa kina mana kuna lugha ama vifungu vya Sheria.
Hiyo franchise mana yake uko committed kutoa huduma zao tu na wala hakuna aina yoyote ya biashara utaweka ndani ya hiyo duka utakalofungua.
Pango,mfanyakazi ama wafanyakazi na mtaji Wa biashara ni juu yako wao wanakuwezesha kununua huduma zao na kuziuza kwa walaji.
Mfano Airtel money unawekea mawakala wengine float,unasajili line na Ku swap line,unauza vocha na simu zao na kuhudumia wateja Wa kawaida Wa Airtel money.

Cha ajabu eneo ni dogo ila wamewapa uwakala huo kama watu watano. Anauliza kama wangekuwa wao wenyewe kwa gharama zao wangeweza kufungua hizo ofisi tani kwa mkupuo na wakalipa hizo gharama .
Hii kitu katika taratibu za biashara imekaaje wanajukwaa msaada tumsaidie huyu ndugu yetu.
Mana wana utaratibu kwanza una deposit Hela kama 1M I.e Milioni moja kwa akaunti yao kuu ya Airtel ndo wanakushughulikia kwa kupambia ofisi kwa kuweka aluminium na teller desk za kuhudumia wateja.

Nina imani kulileta hili jambo hapa kuna mawazo chanya mana hii ni forum ya great thinkers.
Pia ninaomba tusameheane mwandiko tujikite katika mantiki ama logic .
Asanteni wanajukwaa Sina zaidi ni huko tu.
 
Back
Top Bottom