Airtel na TTCL nini kimetokea?

neo1

JF-Expert Member
Sep 1, 2013
577
838
Habari zenu wanajamvi??

Kama mmesikia kuwa TTCL imerudisha hisa zake za 35% toka celtel au Airtel Tanzania.

Okey me naomba kuelezwa nan alikuwa hisa kwa mwingine...

Wataalam wa mambo wanasema izo hisa zilizokuwa kwa Airtel ulikuwa ni ubia ambao kwa ajili ya TTCL kuwa ndani ya Airtel na wameenda mbali zaid kusema sasa serikali haina umiliki wa hisa hata 1 ndani ya kampuni kubwa kama Airtel

Ila kwa upande mwingine wanasema hizo ni hisa za Airtel ambazo zilikuwa ndani ya TTCL na zilikuwa zinawanyima TTCL uwezo wa kuingia kwenunye soko la GSM Sababu anaonekana tayari anafanya biashara ya GSM kwenye Airtel... Hivyo ina mnyima haki ya kuanzisha na kuendeleza GSM

Maswali nan alikuwa anapata gawio kutoka kwa mwenzake??... Je Airtel walikuwa wanalipa gawio kwa TTCL??

Je airtel walikuwa wanachangia iyo asilimia 35 ya maboresho ya TTCL.

Je TTCL ilikuwa kwenye bodi Ya maamuz kwenye Airtel.

Mimi sifaham kilichotokea, wajuvi tueleweshane
 
yaan hapo ndo wametuacha...nini kimetokea The Boss saidia hapa maana hata sielew,
mara ya kwanza walisema ukiritimba sasa wamenunua hisa kwa thaman ya dollar m7.7 ni hela nyingi saana kulipia kwa ghalama kwa kitu ambacho kilikuwa hakina uzalishaji wa faida hiyo.
ukisoma vizuri kwenye makala tofauti wanaeleza ilikuwa inajiendesha kwa hasara.
kwa nn hasara apate TTCL wakati mbia mwenza anatengeneza faida kwenye Airtel...
je wale wakaguz wa mahesabu hawaoni.
kwa nini TTCL wenyewe hawajauza hisa kwenye soko la hisa kama ambavyo sheria ya makampuni ya sim ilipitishwa mwaka 2013
me bado sijaelewa nini kimetokea
 
Kwa wadau wa mambo,

Nadhani sasa tujue nini imetokea,

Maana leo maneno ya JPM yamebadirisha upepo wote.

wajuvi wa mambo.
 
Hivi Rostam na Lowassa kuna mtu mwenye hisa huko???.. Naona harufu ya siasa za kukomoana.kilichomkuta Manji kinawafata wengine...

Daah hili lisukuma shamba kweli
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom