The Son
JF-Expert Member
- Jul 30, 2012
- 459
- 58
Wakala amepewa pesa atume kwenye namba f'lani, aliyempa akishuhudia, baadae...aliyetumiwa hajaona chochote, wakala? Anadai kwake salio limepungua hivyo pesa ilikwenda, SMS ya ushahidi? Hakuna. "Wapigie airtel customer care kwenye namba 100", hakuna maelezo yaliyonyooka, kila unayefanikiwa kuzungumza nae ana maelezo tofauti na mwenzie kuhusu hiyo issue moja, na wanakata Tsh 54/- kwa kila muito baada ya ule wa mwanzo. Elfu hamsini (50,000/-) haziko kwa wakala, haziko kwa aliyetumiwa. Ziko wapi? Na kama mtandao ulizingua, hazirudi kwa wakala?